Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

23 Novemba 2023

19:09:40
1414372

70% ya vijana Marekani wanapinga Biden kuikingia kifua Israel

Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa, aghalabu ya vijana nchini humo hawaungi mkono msimamo wa Rais Joe Biden kwa mashambulizi ya mabomu, jinai za kivita na uporoaji wa ardhi unaofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Palestina.

Utafiti huo uliofanywa na shirika la habari la NBC unaonyesha kuwa, asilimia 70 ya vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 34 wanapinga hatua ya Biden ya kuikingia kifua Tel Aviv.

Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 56 ya wapiga kura nchini humo wanapinga msimamo wa Biden wa kuutetea na kuunga mkono utawala wa Kizayuni.

Hata hivyo asilimia 34 ya waliohojiwa kwenye utafiti huo wa maoni wanasema wanaunga mkono namna Biden anavyoshughulikia mgogoro wa Israel na Palestina.

Kadhalika matokeo ya utafiti huo wa maoni uliofanywa na shirika la habari la NBC yanaonesha kuwa, ni asilimia 40 tu ya Wamarekani wana mtazamo chanya kwa rais huyo mwenye umri wa miaka 81.Aidha kulingana na takwimu zilizopatikana kutoka Kituo cha Taaluma za Siasa cha Marekani katika Chuo Kikuu cha Harvard na uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni na taasisi ya Harris, kiwango cha umaarufu na uungaji mkono wa wananchi kwa Biden kimepungua. Wiki iliyopita, maelfu ya Wamarekani walikusanyika mbele ya Ikulu ya White House na New York kupinga siasa za Biden za kuunga mkono jinai za utawala wa kibaguzi wa Israel. Uungaji mkono wa kiusalama na kijeshi wa nchi za Magharibi hususan Marekani kwa Israel kwa kisingizio cha kujilinda umeupa utawala huo 'kibali' cha kuendelea kuwaua kikatili watoto na wanawake wa Kipalestina.

342/