Main Title

source : Parstoday
Jumatano

6 Desemba 2023

14:59:05
1417942

Hamas: Madai yasiyo na msingi ya Biden ni kielelezo cha kuporomoka kwake kimaadili

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa, madai yasiyo na msingi ya Rais wa Marekani kuhusu operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa yanaonyesha kuporomoka kwake kimaadili.

Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa, harakati ya Hamas imetangaza katika taarifa yake kwamba: Madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na Rais wa Marekani, Joe Biden, dhidi ya Wapalestina kuhusu eti unyanyasaji wa kingono tarehe 7 Oktoba ni kielelezo cha anguko na kuporomoka kwake la kimaadili.

Taarifa ya Hamas imeongeza kuwa, bwabwaja na tuhuma hizo zisizo na msingi haziwezi kutolewa isipikuwa na Wazayuni na propaganda zao zisizo na thamani yoyote.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina imesema: Kukaririwa uongo huo wa wazi wa Wazayuni, mara hii kutoka mdomoni mwa Joe Biden, kunalenga kuficha jinai za kivita, mauaji ya kimbari na mauaji ya halaiki yanayofanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina na kuhadaa maoni ya umma.  

Katika taarifa hiyo Hamas imevitaka vyombo vya habari kuwa makini na uongo mpya wa Wazayuni, ikikumbusha uwongo wao uliofichuliwa hapo awali kama madai yao kukatwa vichwa watoto wa Israel au eti kutumia kijeshi Hospitali ya Shafaa.

Jumamosi, tarehe 7 Oktoba 2023, makundi ya wapigania uhuru ya Palestina yalianzisha operesheni ya kushtukiza iliyopewa jina la "Kimbunga cha Al-Aqsa" kutokea Ukanda wa Gaza (kusini mwa Palestina) dhidi ya vituo na kambi za kijeshi za utawala ghasibu wa Israel ili kulipiza kisasi na kufidia uhalifu na jinai zinazofanywa na utawala huo. Ili kulipiza kisasi cha operesheni hiyo, Israel inaendelea kufanya mauaji ya kikatili ya raia wa Palestina na hadi sasa imeua zaidi ya watu elfu 16 eneo la Ukanda wa Gaza. 

342/