Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

9 Desemba 2023

19:02:24
1418663

Kuchukizwa wananchi wa Marekani na uungaji mkono wa Washington kwa jinai za Israel huko Gaza

Waandamanaji nchini Marekani wamekusanyika mbele ya nyumba ya Waziri wa Mambo ya Nje wakilalamikia uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza.

Anthony Blinken Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amekuwa akitoa matamshi ya mara kwa mara akiunga mkono jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza na kujaribu kuwaonyesha walimwengu kuwa Wazayuni ni wahanga walio na haki ya kujilinda.

Ijumaa kundi la waandamanaji wanaounga mkono Palestina walikusanyika mbele ya nyumba ya Anthony Blinken huko Washingtone na kumtuhumu kwa kuunga mkono mauaji ya kimbari ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina.

Waandamanaji walipiga nara dhidi yake akiwa anatoka nyumbani kwake mjini humo. 

Huku wakipeperusha bendera wakiwa wamevalia hafia za Kipalestina waandamanaji hao pia wametaka kusimamishwa misaada ya kijeshi ya Marekani kwa Israel.

Waandamanaji hao dhidi ya Wazayuni wamesisitiza umuhimu wa kukomeshwa vita na kudumishwa amani katika Ukanda wa Gaza.

Uungaji mkono wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni unapelekea kushadidi siku baada ya siku jinai za utawala huo katika ukanda huo.

Ijumaa, ikiwa ni katika moja ya hatua zake za upendeleo kwa Israel dhidi ya wananchi wa Gaza, Marekani ilipinga kwa kura ya veto, azimio lililopendekezwa na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

342/