Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

9 Desemba 2023

19:03:02
1418665

Marekani yatumia kura ya veto kupinga muswada wa kusitisha vita Gaza

Marekani imetumia kura ya veto kupinga muswada wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliokuwa ukitaka kusitisha vita katika Ukanda wa Gaza.

Hatua hiyo ya Marekanii kwa mara nyingine tena imekwamisha juhudi za kimataifa za kusitisha mauaji ya kinyama yanayofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.

Muswada wa azimio hilo la Umoja wa Mataifa uliungwa mkono na wanachama 13 kati ya 15 wa Baraza la Usalama. Uingereza ambayo ni mwanachama mwingine wa kudumu wa Baraza la Usalama ilijizuia kupiga kura.

Robert Wood, Naibu Balozi wa Marekani katika  Umoja wa Mataifa, amelikosoa baraza hilo baada ya kura hiyo, akidai kwamba, eti limeshindwa kulilaani shambulizi la Hamas huko Israel pamoja na kutambua haki ya Israel ya kujilinda.Kadhalika amedai kuwa, eti kusitisha mapigano kutatoa mwanya kwa Hamas kuendelea kulitawala eneo la Gaza na kufanya mashambulizi mengine ya kigaidi.Marekani inapinga muswada wa azimio la kusitisha vita huko Gaza licha ya indhari na maonyo kadhaa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba hali inazidi kuwa mbaya katika Ukanda wa Gaza. Hatua hiyo ya Marekani inakuja siku moja tu, ambao katika hatua isiyo ya kawaida, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitumia mamlaka aliyopewa kisheria kupitia kifungu cha 99 cha Hati ya Umoja wa Mataifa kulishinikiza Baraza la Usalama la umoja huo lianzishe haraka usitishaji vita huko katika Ukanda wa Gaza. Kifungu hicho, ambacho kimetumika mara 9 pekee katika historia nzima ya Umoja wa Mataifa, kinamruhusu katibu mkuu wa umoja huo kuwaalika wajumbe wa Baraza la Usalama kwenye mkutano wa dharura na kuwataka wachukue hatua za dharura kwa ajili ya kukabiliana na kile anahisi kinahatarisha "usalama na amani ya dunia."

342/