Main Title

source : Parstoday
Jumapili

10 Desemba 2023

16:13:55
1418960

Guterres: Sitaacha kusisitiza ulazima wa kusitishwa vita huko Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema hataacha kusisitiza usitishwaji wa mapigano kwa sababu za kibinadamu huko katika Ukanda wa Gaza.

Antonio Guterre ameyasema hayo baada ya kushindwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha azimio la kusitisha mapigano huko Gaza kutokana na kura ya veto ya Marekani.

Baada ya kitendo cha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa cha kutumia Ibara ya 99 ya Hati ya Umoja wa Mataifa, ambayo ni nadra sana kutumiwa na Katibu Mkuu wa umoja huo kwa ajili ya  usitishaji vita wa mara moja huko Gaza, ambayo imekabiliwa na kura ya veto ya Marekani, Antonio Guterres amesisitiza kwamba hataacha kusisitiza udharura wa kusitishwa mapigano huko Gaza.

Ibara ya 99 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambayo imetumika mara 9 pekee katika historia ya umoja huo, inamruhusu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kubwa zaidi duniani kuwaita wajumbe wa Baraza la Usalama kwenye mkutano wa dharura wakati anapohisi kwamba "amani na usalama wa dunia" uko hatarini na kuwataka wachukue hatua za haraka kuhusu suala hilo.Akizungumza katika mkutano wa Doha, mji mkuu wa Qatar, Guterres amekiri kwamba "vita vya Gaza vimedhoofisha uaminifu na uhalali wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa." Muswada wa kusitishwa mashambulizi ya Israel dhidii ya watu wa Ukanda wa Gaza ulipigiwa kura usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama uliofanyika New York, na kupasishwa na wanachama 13 kati ya 15 wa baraza hilo. Marekani imeupinga kwa kura ya veto huku Uingereza ikijizuia kupiga kura. Muswada huo ulitoa wito wa "kusitishwa mapigano mara moja kwa sababu za kibinadamu" na kuungwa mkono na nchi za Kiarabu na Kiislamu. Antonio Guterres aliamua kutumia Ibara ya 99 ya Hati ya Umoja wa Mataifa baada ya hali ya watu wa Gaza kuwa mbaya sana kutokana na mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel katika eneo hilo la Palestina. Takwimu zinaonyesha kuwa, karibu Wapalestina elfu 20, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake, wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 42,000 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya kikatili ya Israel.

342/