Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

11 Desemba 2023

14:27:53
1419333

Kulaaniwa kimataifa veto ya Marekani dhidi ya azimio la Baraza la Usalama la kusitisha vita vya Gaza

Kitendo cha kinyama na cha kijinai cha Marekani cha kulipigia kura ya veto azimio la kusitisha vita Gaza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kimeendelea kulaaniwa kimataifa.

Anwar bin Ibrahim, Waziri Mkuu wa Malaysia amesema asikitishwa mno na utendaji wa Marekani ambao hadi sasa ungali unatetea bila kikomo mauaji dhidi ya watoto katika Ukanda wa Gaza na amelaani vikali hatua hiyo ya Washington. Waziri Mkuu wa Malaysia amesisitiza kuwa: Ulimwengu mzima umelaani vitendo vya Israel na kuandamana pia dhidi ya utawala huo, lakini bado tu Marekani inaendelea kupuuza haki za binadamu, mimi ninalalamikia hili na kwa kweli ninimehuzunishwa mno na jambo hili.

Malaysia ni moja ya nchi muhimu za Kiislamu ambazo daima zimekuwa zikiwaunga mkono watu wa Palestina na malengo yao matukufu.

Marekani, ambayo ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ijumaa iliyopita ilipinga azimio lililopendekezwa na Imarati (UAE) la kuanzisha usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

Muswada huo ulipigiwa kura katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama uliofanyika usiku wa kuamkia leo, na kupasishwa na wanachama 13 kati ya 15 wa baraza hilo. Marekani imeupinga kwa kura ya veto huku Uingereza ikijizuia kupiga kura. Muswada huo ulitoa wito wa "kusitishwa mapigano mara moja kwa sababu za kibinadamu" na kuungwa mkono na nchi za Kiarabu na Kiislamu.

Azimio lolote linahitaji kwa akali kura 9 ili kupasishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bila kupingwa kwa kura ya veto ya wajumbe 5 wa kudumu wa baraza hilo yaani Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia na China.Katika radiamali yake kwa hatua hiyo ya Marekani Anwar Ebrahim amesema: Ningependa, kwa niaba ya serikali ya Malaysia, kulaani vikali na kwa nguvu zote hatua ya Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kupinga usitishaji vita huko Gaza.

Wakati huo huo, serikali ya Pakistan imetoa taarifa rasmi na kutangaza kwamba, imesikitishwa sana kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halikutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza tena kutokana na kura ya turufu ya Marekani, na inalaani kitendo hiki. Wakati huo huo, vyama vya kidini vya Pakistan vilifanya mkutano ambapo sambamba na kuunga mkono wananchi wa Palestina vililaani kura ya turufu ya Marekani dhidi ya azimio la kusitisha mapigano huko Gaza. Morteza Haider, mtaalamu wa masuala ya kisiasa, anasema:

Uungaji mkono wa Marekani kwa ajili ya kuendelea jinai za Wazayuni huko Gaza si suala geni, na kwa hakika, katika miongo saba iliyopita, Wazayuni wameendeleza jinai zao kwa uungaji mkono kamili wa Marekani, na lililo muhimu katika hali ya hivi sasa ni kwamba Marekani imesimama dhidi ya walimwengu ambao wanataka kuhitimishwa jinai katika Uukanda wa Gaza.



342/