Main Title

source : Parstoday
Jumatano

13 Desemba 2023

11:02:05
1419864

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS yaitambua rasmi serikali ya Niger

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeitambua rasmi serikali mpya ya Niger ikiwa ni katika kulegeza misimamo yake ya kisiasa na kiuchumi kuhusiana na nchi hiyo.

Omar Alieu Touray Mkuu wa Tume ya ECOWAS, amesema katika mkutano wa jumuiya hiyo huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria kwamba timu ya wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wanafanya mazungumzo na serikali ya kijeshi ya Niger ili kukabidhi madaraka katika kipindi kifupi.Wakuu wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi walikata uhusiano wao na Niger muda mfupi baada ya kuingia madarakani jeshi na hata kutishia kuingilia kijeshi ili kumrejesha madarakani rais aliyeng'olewa madarakani wa nchi hiyo Muhammad Bazum.

Mnamo Julai 26, 2023, walinzi wa rais wa Niger walifanya mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo, Mohamed Bazoum, na kumchagua Abdelrahman Tiani mkuu wa walinzi wa rais, kuwa mkuu wa baraza la mpito.

Baraza la Kijeshi la Niger lilichukua madaraka katika nchi hiyo huku likitaka kuondoka vikosi vya kigeni hasa vya Ufaransa huko Niger na kukomeshwa uingiliaji wa Paris katika masuala ya nchi hiyo. Msimamo huo ulipelekea utawala wa kijeshi kupata uungaji mkono mkubwa wa wananchi.  Ndani ya Niger, mamia ya wafuasi wa baraza la kijeshi waliandamana mbele ya ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu, Niamey. Walimchukulia Bazem kuwa mwitifaki wa nchi za Magharibi hasa Ufaransa na huku wakiunga mkono kuondolewa kwake madarakani, walitaka Wamagharibi wasitishe uingiliaji katika mambo ya ndani ya nchi yao.



342/