Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

16 Desemba 2023

13:14:13
1420712

Wajerumani 27 kuhukumiwa kwa tuhuma za ugaidi na jaribio la kupindua serikali

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wametangaza kwamba kesi inayowakabili watu 27, akiwemo aliyekuwa mbunge wa nchi hiyo, kwa tuhuma za kupanga mapinduzi dhidi ya serikali itaanza kusikilizwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa televisheni ya Euronews, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Ujerumani imetangaza kuwa, watu 27 akiwemo mbunge wa zamani wa Bunge la nchi hiyo mwenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia, watahukumiwa hivi karibuni kwa tuhuma za ugaidi kutokana na jaribio la kupindua serikali.

Euronews imeripoti kuwa, jaribio la kundi hili la kutaka kupindua serikali ya Ujerumani lilifichuliwa mwaka jana, na baada ya hapo idadi kubwa ya wahusika ilikamatwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwendesha Mashtaka wa Ujerumani, washukiwa 9 wa kesi hii ambao wote ni raia wa Ujerumani, wanatuhumiwa kuwa wanachama wa "shirika la kigaidi" lililoanzishwa Julai 2021 kwa lengo la "kuipindua serikali ya Ujerumani kwa shambulio la silaha."

342/