Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

18 Desemba 2023

16:33:50
1421300

Baada ya kushambuliwa kanisa, Papa Francis asema: Mashambulizi ya Israel huko Ghaza ni ugaidi

Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema kuwa, mashambulizi ya kikatili yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza ni ugaidi.

Shirika la habari la FARS limemnukuu Papa Francis akisema hayo katika hotuba yake ya jana Jumapili baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kumuua mama na binti yake kwenye kanisa moja huko Ghaza.

Akiendesha misa ya kila wiki huko Vatican, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amesema: Nimekuwa nikipokea habari mbaya na za kusikitisha sana kuhusu Ghaza.

Ameongeza kuwa, raia wasio na silaha wanashambliwa kwa makombora na risasi. Mashambulizi hayo yanafanyika katika makazi ya raia huko Khan Yunus maeneo ambayo hakuna hata hao wanaodaiwa ni magaidi. Watoto, wanawake, wagonjwa na vilema ndio wanaoshambuliwa.Juzi Jumamosi pia, Askofu Mkuu wa mji wa Baytul Muqaddas alitoa tamko akisema kuwa, tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha vita tarehe 7 Okroba, familia za Wakristo wa Ghaza zimekimbilia makanisani na kwenye mahandaki, lakini wanajeshi wa Israel wameshambulia eneo la kanisa ambalo lilikuwa limewapa hifadhi vilema 54. Katika tamko lake hilo, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki la Baytul Muqaddas ambaye anasimamia makanisa yote ya Kikatoliki ya Cyprus, Jordan, Ghaza na ardhi nyingine za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina bandia la Israel, amelaani jinai ya wanajeshi wa Israel ya kumuua mama na binti yake ndani ya kanisa huko Ghaza. Tarehe 7 Oktoba wanamapambano wa Palestina walitoa pigo kubwa la kihistoria na la kijeshi na kiusalama kwa utawala pandikizi wa Israel kupitia operesheni ya #Kimbunga_cha_al-Aqsa. Baada ya Israel kushindwa kukabiliana na wanamapambano wa Palestina kwenye medani za vita, imeamua kushambulia kinyama kila kitu yakiwemo makanisa, Misikiti, mahospitali, maskuli na maeneo yote ambayo sheria za kimataifa zimepiga marufuku kushambuliwa katika mazingira yoyote yale. 

342/