Main Title

source : Parstoday
Jumatano

20 Desemba 2023

15:53:52
1421988

Ayatullah Ramezani: Sheikh Zakzaky ni mfano halisi wa mujahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as) amekutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kusema kuwa, Sheikh Zakzaky ni mfano halisi wa Mujahid fi Sabilillah (mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu).

Ayatullah Reza Ramezani, akielezea kufurahishwa kwake na kukutana na Sheikh Ibrahim Zakzaky na akizungumzia siku ambazo alikabiliwa na hujuma zisizo za kiutu na zilizo mbali na urijali na kufungwa jela, amemtaja Sheikh Zakzaky kuwa "mwanamageuzi wa kifungoni".

Huku akithamini juhudi za Sheikh Zakzaky nchini Nigeria za kueneza utamaduni wa Kishia, Ayatullah Ramezani amesisitiza kuuwa, Sheikh Zakzaky mfano halisi wa Mujahid Fi sabilullah na kueleza matumaini yake kuwa juhudi na njia za Sheikh Zakzaky zitaendelea.

Katika sehemu ya kikao hicho, Ayatullah Ramezani ameelezea baadhi ya shughuli za Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as) na kusema: Kuna idara mbalimbali katika jumuiya hilo zikiwemo Ensaiklopidia ya WikiShia yenye lugha 22, shirika la habari la Ahlul Bayt (AS) - Abna - katika lugha 27, Kanali ya satelaiti wa Thaqalayn na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Ahlul-Bayt (as) ambapo wanafunzi kutoka mataifa 29 wanasoma taaluma mbalimbali.Kwa upande wake Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Waislamu wa Nigeria waliathiriwa pakubwa na mapinduzi hayo na vuguvugu la Istbasar (kuingia katika madhehebu ya Shia) likaibuka, lakini maadui nchini Nigeria walianza propaganda na shutuma dhidi ya Shia na shutuma hizo ziliongezeka hasa baada ya mauaji ya Zaria. Katika shambulio lililofanywa na jeshi la Nigeria Disemba 12, 2015, inakadiriwa wanachama zaidi ya 1,000 wa harakati ya Kiislamu ya Nigeria, aghalabu wakiwa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia, waliuawa kwa kufyatuliwa risasi na jeshi la serikali ya Abuja. Miongoni mwa waliouawa walikuwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

342/