Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

22 Desemba 2023

19:36:43
1422552

Rais Putin atoa onyo kali kwa viongozi wa nchi za Magharibi

Rais wa Russia amesema kuwa umefika wakati sasa kwa Marekani na nchi za Magharibi kuachana na fikra ya kusambaratika Russia.

Baada ya vita kuanza huko Ukraine mwezi Februari mwaka jana nchi za Magharibi ziliilaani Moscow, zikashadidisha vikwazo vya kiuchumi na kuliweka katika ajenda yao ya kazi suala la kuiunga mkono kwa pande zote Kyiv yaani kisasa, kifedha na kisilaha. Katika medani ya vita, Russia imeweza kudhibiti asilimia zisizopungua 20 za ardhi ya Ukraine licha ya misaada ya  nchi za Magharibi kwa nchi hiyo. 

Rais Vladimir Putin wa Russia alisema jana katika mkutano wa Baraza la Maendeleo ya Kistratejia na Miradi ya Taifa la nchi hiyo kwamba: "Ningependa kuzingatia kuwa hatujiweki mbali na Amerika yaani kuanzia Amerika ya Kaskazini, Marekani  na Canada."  

Raisi wa Russia hivi karibuni alisema kuwa Moscow inaboresha silaha zake za nyuklia na kuviweka vikosi vyake vya kimkakati vya nyuklia katika utayari wa kiwango cha juu. 

Hadi sasa Russia na nchi nyingine zimewasilisha mapendekezo ya amani ambayo hata hivyo yamekabiliwa na jibu hasi la Kyiv na washirika wake wa Magharibi. 

342/