Main Title

source : Parstoday
Jumapili

24 Desemba 2023

16:26:05
1423280

Uhispania, Italia, Ufaransa na Australia zakataa kujiunga na muungano wa majini wa Marekani

Nchi tatu za Ulaya na Australia zimekataa kujiunga na muungano wa wanamaji katika Bahari Nyekundu ulioanzishwa na Marekani eti kukabiliana na harakati ya Ansarullah na Jeshi la Majini la Yemen ambalo limepiga marufuku kupita meli zote za Israel katika lango bahari la Bab al-Mandab kwenye Bahari Nyekundu.

Serikali ya Marekani ilitangaza siku kadhaa zilizopita kwamba imeanzisha muungano wa kimataifa wa baharini uliopewa jina la "Operation Prosperity Guardian" ili kulinda njia za meli za kibiashara katika Bahari Nyekundu na kukabiliana na mashambulizi ya harakati ya Ansarullah. Nchi kadhaa zimeukaribisha muungano huo, ilhali aghlabu ya nchi duniani hata washirika wa karibu wa Marekani na Israel wamekataa kujiunga na muungano huo. 

Siku chache zilizopita Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, alikuwa ametangaza rasmi kuwa, nchi za Bahrain, Uingereza, Ufaransa, Italia, Uholanzi, Norway, Seychelles na Uhispania zimejiunga katika muungano huo. 

Sasa baada ya tangazo la kujiondoa nchi tatu muhimu za Ulaya katika muungano wa wanamaji wa Marekani katika Bahari Nyekundu, itakuwa vigumu sana kufikiwa malengo ya Washington hususan kukabiliana na mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Yemen dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na meli zinazoelekea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.Wakati huo huo, tangazo la kujiondoa nchi tatu wanachama wa NATO wa Ulaya katika muungano wa wanamaji wa Marekani linaonyesha msimamo wa nchi hizo wa kutokuwa na imani na Washington. Vilevile hatua hiyo inatajwa kuwa ni aina fulani ya malalamiko na upinzani dhidi ya sera za Marekani za kuuhami na kuukingia kifua utawala unaoendelea kuua watoto wa Israel na kupinga suala la kusitishwa vita vya umwagaji damu huko Gaza. Kwa upande wake, harakati ya Ansarullah na jeshi la Yemen limetangaza kuwa, litaendelea kushambulia meli za kibiashara za Israel madhali utawala huo haramu unaendelea kufanya jinai na kuua raia wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza. ​Ansarullah imeongeza kuwa: Muungano uliotangazwa na Marekani ni sehemu muhimu ya hujuma dhidi ya watu wa Palestina, Gaza na Umma wa Kiarabu na Kiislamu.

342/