Rais Alexender Lukashenko wa Belarus alisema jana huko St. Petersburg katika hotuba yake katika Mkutano wa Jumuiya ya Kiuchumi inayoongozwa na Russia bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya silaha hizo zilizotumwa au mahali zilipopelekwa kwamba: Russia ilikamilisha zoezi la kuikabidhi Belarus silaha za nyuklia za kitaktiki mnamo mwezi Oktoba mwaka huu. Alipoulizwa kwa nini shehena ya silaha hizo imekabidhiwa nchi yake, Rais Alexender Lukashenko pia amesema: Hatua hiyo imechukulikwa ili kuzuia uchokozi wa Poland ambayo ni mwanachama wa Muungano wa Nato. Russia ilisisitiza kabla ya kujiri zoezi la kuipatia Belarus silaha za nyuklia za kitaktiki kwamba nchi hiyo ndiyo itakayosimamia matumizi ya silaha hizo.
342/