Main Title

source : Parstoday
Jumanne

26 Desemba 2023

17:15:28
1423956

Papa Francis ataka kusitishwa vita Ukanda wa Gaza

Kiongozi wa Wakristo wa Katoliki duniani jana alitoa hotuba katika Sikukuu ya Krismasi kwa mnasaba wa kuzaliwa Nabii Isa Masih (a.s), na kutaka kusitishwa vita Ukanda wa Gaza.

Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani jana alisoma ujumbe wake huo mbele ya maelfu ya waumini wa Kikristo wa Katoliki waliokuwa wamekusanyika katika maidani ya St. Peter huko Vatican Italia na kutoa wito wa kusitishwa vita katika Ukanda wa Gaza na kupatiwa ufumbuzi hali ngumu wanayopitia Wapalestina wa eneo hilo kupitia kufunguliwa njia za kufikisha huko misaada zaidi ya kibinadamu.  

Umoja wa Mataifa hivi karibuni ilitangaza kuwa hali ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza ni mbaya sana baada ya kupita karibu miezi mitatu tangu kuanza mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika ukaknda huo; na kusema hadi sasa asilimia 85 ya wakazi wa Gaza wamekuwa wakimbizi. 

Utawala wa Kizayuni umeanzisha mauaji makubwa ya kikatili huko Ukanda wa Gaza na katika eneo la Ukingo wa Magharibi dhidi ya raia wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina tangu Oktoba 7 mwaka huu kwa uungaji mkono na himaya ya pande zote ya nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani. Wapalestina 20,424 wengi wakiwa ni wanawake na watoto wameuawa shahidi na wengine elfu 54, na 36 kujeruhiwa tangu utawala haramu wa Israel uanzishe mashambulizi ya kikatili huko Gaza. 

342/