Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

28 Desemba 2023

15:36:05
1424604

Radiamali dhidi ya uamuzi mbovu wa Papa kuhusu ndoa za watu wa jinsia moja kanisani

Katika hali ya kutatanisha na ambayo haijawahi kushuhudiwa tena huko nyuma, Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametoa ruhusa rasmi kwa makasisi kufanya sherehe na kubariki ndoa za watu wa jinsia moja katika kanisa hilo.

Katika barua aliyowaandikia makadinali wawili wa kihafidhina na kuchapishwa na Vatican karibuni hivi, Papa Francis amewaambia makadinali kwamba, ili kutochanganywa sherehe za ndoa za watu wa jinsia moja na zile za ndoa takatifu, wanaweza kufanya sherehe hizo na kuwatakia baraka katika maisha yao wanandoa wa aina hiyo. 

Barua hiyo imebainisha kuwa, neno 'baraka' lina ufafanuzi mpana katika Biblia, na kuwa watu wanaotaka kuwa na uhusiano mzuri na Mwenyezi Mungu na kupata upendo na huruma yake hawapaswi kuwekewa masharti yoyote.

Waraka huo mpya wa Vatican ni hatua ya hivi karibuni zaidi ya Papa Francis inayoonyesha kulegeza msimamo Kanisa Katoliki kuhusu watu wa jinsia moja au kwa ibara nyingine LGBT.

Ruhusa hiyo imetolewa na Papa katika hali ambayo siku zote Vatican imekuwa ikiamini kwamba ndoa ni kifungo kisichopasa kuvunjwa kati ya jinsia mbili za mwanaume na mwanamke tu, na ndio maana imekuwa ikipinga ndoa za watu wa jinsia moja. Wakati huo huo wengi wa Wakristo wa Kikatoliki wanautaja ushoga kuwa dhambi kubwa na kuamini kuwa haiwezekani kuwaombea wahusika rehema na baraka za Mwenyezi Mungu.

Uamuzi huo mpya wa Papa umezua hasira kubwa kati ya wafuasi wake. Luigi Casalini, mmoja wa wanablogu wa Kikatoliki, pamoja na kukosoa uamuzi huo wa Papa Francis ameandika: 'Waraka huo ni aina ya uzushi na Kanisa linakaribia kuporomoka.'

Ushoga na usagaji umepewa umuhimu mkubwa katika uga wa siasa za kimataifa katika miaka ya hivi karibuni, ambapo nchi nyingi za Magharibi kwa kutoa kipaumbele kwa suala hilo zinachukulia marufuku dhidi ya kitendo hicho cha kuchukiza kuwa inakinzana na misingi ya uhuru wa mtu binafsi na haki za binadamu. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo zimekuwa zikizishinikiza kwa njia mbalimbali nchi ambazo hazikubaliani kisheria na uchafu huo, mashinikizo ambayo yamekuwa yakitekelezwa kwa mbinu tofauti ikiwa ni pamoja na kuzikatia misaada ya kifedha, kuziwekea vikwazo na kuzishinikiza kisiasa. Katika radiamali yake kuhusiana na uamuzi wa hivi karibuni wa serikali ya Uganda wa kupiga marufuku na kuwaadhibu wanaohusika na vitendo vya ushoga na usagaji, Rais Joe Biden wa Marekani alitishia kutazama upya vipengele vyote vya uhusiano wa nchi hiyo na Uganda.

Ukweli ni kuwa, kwa sasa, mashirika mengi ya kimataifa, kitaifa na ya ndani ya nchi kwa msaada wa taasisi za kisiasa yanajaribu kuarifisha ushoga na usagaji kama mtindo mpya wa maisha na "mfumo mpya" kati ya mifano mingine mpya kwa ajili ya mwanadamu wa leo. Suala hilo bila shaka linaweza taratibu kuleta mfumo mpya wa kijamii na kudhihirisha ulimwenguni maadili maovu yanayofuatiliwa na nchi za Magharibi kwa madhara ya jamii ya mwanadamu.

Siasa hizo pia zimepelekea kuongezeka mashinikizo ya kisiasa na kijamii dhidi ya makanisa ambayo kwa miaka mingi yamekuwa yakihubiri kuimarishwa maadili mema katika jamii, kwa kadiri kwamba inaonekana kuwa Papa Francis naye amenaswa katika mashinikizo hayo na hatimaye kumpelekea aruhusu kufanyika vitendo vichafu vya ndoa za watu wa jinsia moja kanisani. Mwaka 2018 Papa Francis alitahadharisha na kudai kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kuenea vitendo vya ushoga na usagaji miongoni mwa viongozi na wafuasi wa Kanisa Katoliki. Kwa kuzingatia hali hiyo, tangazo la Papa mwenyewe kutoa kibali kwa makasisi kubariki na kuruhusu kufanyika kanisani harusi za kuchukiza za watu wa jinsia moja, limeamsha hasira ya wengi duniani na hasa katika nchi za Kiafrika ambazo zinapinga vikali kuruhusiwa uchafu huo kanisani.