Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

29 Desemba 2023

18:22:52
1424810

Russia: Kuipindua serikali ya Kiev ni "lengo muhimu na lisiloepukika" la operesheni za kijeshi Ukraine

Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Russia ametangaza kuwa kupinduliwa serikali ya Kiev ni "lengo muhimu zaidi na lisiloweza kuepukika" la operesheni za kijeshi za nchi hiyo nchini Ukraine.

Dmitry Medvedev, ameyasema hayo katika mahojiano na shirika la habari la RIA Novosti, alipojibu swali kuhusu matarajio ya mazungumzo ya amani kati ya Moscow na Kiev, ambapo amesema, operesheni za kijeshi nchini Ukraine zitaendelea mwaka ujao.

Medvedev ameongeza kuwa, kupinduliwa serikali inayoungwa mkono na nchi za Magharibi ya Ukraine inayoongozwa na Volodymyr Zelensky ni lengo ambalo halijatangazwa lakini ndilo "lengo muhimu zaidi na lisiloepukika" la operesheni za kijeshi za Russia nchini Ukraine.

Rais huyo wa zamani wa Russia amesisitizia kwa kusema: Odessa, Dnipropetrovsk, Kharkiv, Nikolaev na Kiev ni miji ya Russia kama ilivyo miji mingine mingi ambayo iko chini ya uvamizi wa muda (wa serikali ya Ukraine).Medvedev amesema pia kuhusu mazungumzo ya amani kwamba: Russia, kinyume na viongozi wa Ukraine, haijawahi kulikataa hilo, lakini Moscow haina muda ulioainishwa kwa ajili ya mazungumzo, na mchakato huo unaweza ukaendelea hadi kushindwa kikamilifu majeshi yanayoungwa mkono na NATO nchini Ukraine. Wakati viongozi wa Russia wameshaitaka Ukraine mara kadhaa irejee kwenye meza ya mazungumzo, viongozi wa Kiev wanasisitiza kwamba hakutakuwa na mazungumzo hadi majeshi ya Russia yaondoke nchini humo. Wiki iliyopita, Medvedev alizungumzia hakikisho la usalama lililotolewa na Umoja wa Ulaya kwa Ukraine kuwa ni sawa ni karatasi iliyochanwachanwa na isiyo na matumizi na akasema: Moscow imejiandaa kushambulia kambi yoyote ya kijeshi ya kigeni iliyoko Ukraine.../

342/*