Main Title

source : Parstoday
Jumapili

31 Desemba 2023

17:46:17
1425476

Le Monde: Uwezekano wa kutumia ndege zisizo na rubani katika vita barani Afrika unazua wasiwasi

Gazeti la Ufaransa la Le Monde limechapisha ripoti inayosema kwamba ndege zisizo na rubani zimekuwa tishio kutokana na uwezekano wa kutumiwa sana katika vita barani Afrika, likionyesha kwamba makundi yenye silaha hadi sasa yametumia tu ndege zisizo na rubani kwenye shughuli za upelelezi.

Ripoti hiyo imefichua kwamba uvamizi uliofanywa na kundi la al Shabab kwenye kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Kenya mwaka 2020 huko Manda Bay, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia, ulipangwa kutokana na picha zilizokusanywa kwa kutumia ndege isiyo na rubani ya upelelezi.

Imeongeza kuwa kundi la Daesh (ISIS) Afrika Magharibi limeanza kutumia droni mara kwa mara nchini Nigeria kufuatilia safu ya mbele ya jeshi la nchi hiyo.

Ripoti hiyo imemnukuu Robin Das, mtafiti katika Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Migogoro ya Kisiasa na Ugaidi nchini Singapore, akisema kwamba makundi yenye silaha yanatumia ndege hizi zisizo na rubani kufanya operesheni za upelelezi au kuchukua video za propaganda, na kuongeza kuwa: "Bado hatujaona zikitumiwa katika mashambulizi ya kivita kama ilivyokuwa huko Syria na Iraqi tangu 2016."

Ripoti ya gazeti la Le Monde imesema kuwa "droni za muuaji" - ambazo ISIS ilizitumia kwa kiasi kikubwa dhidi ya muungano wa kimataifa - zina muundo tofauti na wa aina mbalimbali.

Ripoti hiyo imemnukuu mmoja wa maofisa wa Ulaya ambaye hivi karibuni alitumwa katika eneo la Sahel akisema, "Ni suala la muda tu kabla ya teknolojia hii haijatumika katika ardhi ya Afrika."Wakati huo huo, Mkuu wa Vikosi vya Jeshi la Anga la Senegal, Baba Souleymane Sarr, ameelezea hofu yake juu ya utumiaji wa ndege zisizo na rubani katika operesheni za silaha, na kusema kwamba "matumizi makubwa ya vyombo vinayodhibitiwa kwa mbali yamekuwa tishio halisi kwa majeshi yote hata yale yaliyopiga hatua kubwa.”

342/