Main Title

source : Parstoday
Jumapili

31 Desemba 2023

17:47:07
1425477

Maandamano ya waungaji mkono wa Palestina mbele ya Jengo la Biashara la Kimataifa la Marekani

Waungaji mkono wa wananchi madhulumu wa Palestina wamekusanyika mbele ya Jengo la Biashara la Kimataifa la Marekani wakipinga siasa za serikali ya Marekani za kutoa himaya kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yamefanyika mbele ya Jengo la Biashara la Kimataifa la Marekani katika Jiji la New York huku waandamanaji wakibeba mabango yanayomtuhumu Rais Joe Biden wa Marekani kuwa mhusika katika mauaji ya halaiki na kupiga nara za kutaka kukombolewa ardhi za Palestina.

Kabla ya hapo, Wamarekani walijitokeza kwa wingi barabarani katika miji mbalimbali na kueleza mshikamano wao na watu wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza.

Katika maandamano hayo dhidi ya Israel, waandamanaji hao wamewataja Rais Joe Biden" na Anthony Blinken Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuwa wahusika wa moja kwa moja wa mauaji ya kimbari ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza yanayofanywa na utawala wa Kizayuni.Inafaa kukumbusha hapa kuwa tarehe 7 Oktoba 2023, makundi ya muqawama ya Palestina yalifanya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Ukanda wa Gaza dhidi ya maeneo ya utawala wa Israel, na baada ya siku 45 za mapigano na migogoro, tarehe 24 Novemba 2023, usitishwa vita wa siku nne ulianzishwa kwa ajili ya kubadilishana mateka wa vita. Usitishwa vita huo uliendelea kwa siku saba ambapo Desemba 1, 2023, utawala wa Israel ulianza tena mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya Ukanda wa Gaza. Utawala wa Israel umekuwa ukishambulia na kulipua kwa mabomu eneo hilo linalozingirwa kwa takriban miezi mitatu ili kulipiza kisasi shambulizi la kushtukiza la Kimbunga cha Al-Aqsa kwa ajili ya kufidia kushindwa kwake kijeshi na kusimamisha operesheni za muqawama. Tangu yalipoanza mashambulizi hayo ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, Wapalestina 21,320 ambao wengi wao ni wanawake na watoto wameuawa shahidi na wengine 55,603 kujeruhiwa.

342/