Main Title

source : Parstoday
Jumatano

3 Januari 2024

15:15:00
1426310

Haniyeh: Israel itawajibika kwa mauaji ya Arouri

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas, Ismail Haniyeh amesema utawala haramu wa Israel utawajibika kwa mauaji ya afisa mkuu wa harakati hiyo, Saleh al-Arouri, na ameyataja mauaji hayo kuwa ni "kitendo cha kigaidi na ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Lebanon."

Haniyeh aliyasema hayo jana Jumanne, muda mfupi baada ya shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za Israel dhidi ya kitongoji cha kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut lililoua shahidi watu sita akiwemo Arouri.

"Tunaomboleza mauaji ya shahidi wa kiongozi wa mapambano na mtu mkubwa wa kitaifa, Sheikh Saleh Al-Arouri, pamoja na makamanda wa Al-Qassam, Samir Fandi na Azzam Al-Aqra' na mashahidi wengine, kufuatia shambulizi la kiuoga la Wazayuni huko Beirut", amesema Haniyeh.

Ameongeza kuwa: "Mauaji ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Al-Arouri na ndugu zake ni kitendo cha kigaidi na ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Lebanon, na yanapanua wigo wa uchokozi wake kwa watu wetu na taifa letu."

"Utawala wa Kinazi wa Wazayuni unabeba dhima ya uchokozi huu," aliongeza na kusema: "Damu safi ya Sheikh Saleh al-Arouri na ndugu zake imechanganyika na damu ya makumi ya maelfu ya mashahidi wa Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi, na nje ya nchi."

342/