Main Title

source : Parstoday
Jumatano

3 Januari 2024

15:19:28
1426318

Maandamano ya wananchi wa Uturuki ya kupinga vita

Katika muendelezo wa maandamano ya kupinga mauaji ya kimbari ya Waislamu huko Gaza, makumi ya maelfu ya wananchi wa Uturuki wamefanya maandamano makubwa mjini Istanbul kupinga jinai za utawala wa Kizayuni na mauaji ya vijana wa Kituruki kaskazini mwa Iraq katika siku ya kwanza ya mwaka huu mpya wa 2024.

Wananchi na viongozi mbalimbali wa Istanbul Jumatatu ya juzi tarehe Mosi Januari walijitokeza tena mitaani na kulalamikia mauaji ya wanajeshi 12 wa Uturuki kaskazini mwa Iraq na kuendelea mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wasio na hatia wa Gaza.

Maandamano hayo yalifanyika kwa uratibu na mpango wa Jukwaa la Utashi wa Kitaifa katika fremu ya mashirika 308 yasiyo ya kiserikali. Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walipiga nara kama vile, Allah awarehemu mashahidi wetu. Aidha walitoa nara za kuulaani utawala ghasibu wa Israel na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina hususan wa Ukanda wa Gaza ambao wanapitia kipindi kigumu cha masaibu na ukatili wa Israel.Kimya cha namna fulani cha viongozi wa serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan kwa mauuaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza kimepelekea kufanyika maandamano ya mara kwa mara nchini Uturuki katika kipindi cha takribani miezi mitatu tangu kuanza hujuma na mashambulio ya kinyama ya Israel huko Gaza.

Sambamba na maandamano ya wananchi Waislamu wa Uturuki, wachambuzi wa masuala ya kisiasa pia wanapinga siasa za kinafiki za serikali za Magharibi kuhusiana na jinai zinazoendelea Israel na daima wanafichua siasa za serikali za Magharibi. Mapitio ya ya yale yaliyoandikwa kwenye magazeti ya "Sabah", "Hurrit", "Karar", "Yeni Akit" na vituo vingi vya masuala ya utafiti wa maudhui mbalimbali vya Kituruki yanaonyesha kwamba, wachambuzi wengi wa Kituruki wanaamini kuwa, mtazamo wa sasa wa nchi za Magharibi kuhusiana na matukio ya Gaza, hauna uwiano na kaulimbiu zao za haki za binadamu na jinsi walivyolipigia upatu suala la haki za binadamu.

Ahmad Tashgatiren amesema kuhusu mtazamo wa Wamagharibi kuhusu matukio ya sasa ya Gaza:

"Mashambulio ya kinyama ya mabomu dhidi ya Gaza yanaendelea. Kila siku idadi ya vifusi inazidi kuongezeka. Kila siku mauaji ya raia wakiwa na picha za watoto wachanga mikononi mwao yanaongezeka. Lakini uungaji mkono wa Marekani na washirika wake kwa Israel bado unaendelea kuongezeka. Hatua hizo zinamaanisha kwamba viongozi wa nchi za Magharibi, kiutendaji, sio tu kwamba hawana tatizo na mauaji ya Israel huko Gaza, bali pia wana ushindani baina yao wa kumuunga mkono muuaji.