Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

4 Januari 2024

11:52:41
1426681

Kiongozi: Watenda jinai watambue kuwa, wanamapambano wa njia ya Solaimani hawahimili jinai zao

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kufuatia kuuawa shahidi makumi ya wafanya ziara wa Shahid Qassem Soleimani na kusisitiza kuwa, wanaotenda jinai watambue kuwa wanamapambano wa njia ya Soleimani hawawezi kuhimili na kuvumilia jinai zao.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameongeza kuwa, mikono iliyochafuka kwa damu za watu wasio na hatia pamoja na fikra fasidi na zinazozaa shari wa watenda jinai hao ambazo ndizo ziliowapelekea kutumbukia kwenye njia hiyo ovu, wote waelewe kuwa tangu hivi sasa watakumbwa na mawimbi kandamizi ya adhabu za kiuadilifu na watambue pia kuwa, jinai yao hiyo itapata majibu makali. 

Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametumia fursa hiyo kutoa mkono wa pole pamoja na kuwaombea dua za kheri majeruhi wa jinai hizo.

Jana Jumatano tarehe 3 Januari 2024 ilisadifiana na mwaka wa nne wa tangu kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

Jana jioni na wakati wa kumbukumbu hizo kulitokea miripuko miwili ya kigaidi katikati ya kundi la wafanya ziara na kupelekea watu 95 kuuawa shahidi na wengine 284 kujeruhiwa huko katika mji wa Kerman, wa kusini mashariki mwa Iran.

342/