Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

6 Januari 2024

18:46:31
1427199

Mtaalamu wa UN alaani vikali hujuma ya kigaidi katika mji wa Kerman

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran Javaid Rehman amelaani vikali shambulio dhidi ya mjumuiko wa kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa kamanda wa ngazi za juu nchini Iran Shahidi Qassem Soleimani katika mji wa Kerman.

Katika taarifa yake iliyotolewa Ijumaa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR jijini Geneva Uswisi, Rehman amesema wale wote waliohusika na mashambulizi mabaya yaliyotokea siku ya Jumatano nchini Iran na kuua zaidi ya watu 89  lazima wawajibishwe. 

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema: “Mauaji ni mojawapo ya mashambulizi makubwa zaidi dhidi ya maadili ya kimataifa ya haki za binadamu." Aidha ametuma salamu za rambirambi na pole kwa familia za wahanga na wananchi wa Iran.

342/