Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

6 Januari 2024

18:47:06
1427200

Ebrahim Raisi: Usalama wa ukanda huu mzima una deni kwa Luteni Jenerali Soleimani

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, usalama na amani iliyopo leo katika eneo hili inatokana na jihadi kubwa ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

Jumatano tarehe 3 Januari kulitokea miripuko miwili mikubwa ya mabomu kwenye kumbukumbu za mwaka wa nne wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani wakati wafanyaziara walipokuwa katikati ya kumbukumbu hizo mjini Kerman, kusini mashariki mwa Iran. 

Genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) limedai kuhusika na jinai hiyo iliyoua shahidi watu 89 na kujeruhi wengine 284. Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel na waitifaki wake hasa Marekani ndio wahusika wakuu wa jinai hiyo dhidi ya watu wasio na hatia.Shirika la habari la IRIB limemnukuu Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akisema hayo jana Ijumaa wakati wa maziko ya mashahidi wa jinai hiyo huko Kerman na kumshukuru sana Luteni Jenerali Qassem Solaimani kwa jihadi yake kubwa ya kupambana na ubeberu na ugaidi. Amesema kuwa, Shahidi Soleimani alianzisha kambi ya muqawama ya kupambana na uistikbari kwenye eneo hili na kumlazimisha adui kurudi nyuma na kukimbia. Kwa upande wake, Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH alisema jana Ijumaa wakati wa maziko ya mashahidi wa mashambulizi hayo ya kigaidi huko Kerman kuwa, Iran itatoa majibu makali na kwamba, Marekani mbali na kupata pigo huko Iraq, Afghanistan, Lebanon, Syria na Yemen, imefeli pia katika vikwazo vyake vikubwa dhidi ya Iran na sasa hivi haijabakiwa na nukta yoyote ya kiusalama ya kuweza kuwadhibiti Waislamu.

342/