Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Januari 2024

18:17:50
1427471

Nukta 5 za kiuchambuzi katika hotuba ya pili ya Seyyid Hassan Nasrallah mwaka 2024

Seyyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon tarehe 5 Januri katika hotuba yake ya pili katika mwaka huu mpya wa 2024 amejadili vita vya Gaza, kuuawa shahidi Saleh al-Arouri, kiongozi wa Hamas na jinai ya kigaidi huko Kerman.

Mhimili wa kwanza katika hotuba ya Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon kuhusiana na Gaza ulikuwa utendaji wa makundi ya muqawama katika vita hivyo ambavyo vinaendelea kwa zaidi ya miezi 3 sasa.

Ingawa utawala wa Kizayuni umetenda jinai za mauaji ya halaiki katika vita hivyo, lakini pia umepata hasara kubwa kutoka kwa makundi ya muqawama. Makundi ya Muqawama ya Palestina, Lebanon na Yemen yameushambulia utawala wa Kizayuni na kuusababishia hasara mkubwa.

Kuhusiana na hilo, Seyyid Hassan Nasrallah amesema kuwa, katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita wanamqawama wametekeleza zaidi ya operesheni 670 dhidi ya utawala wa Kizayuni, ambapo idadi kubwa ya wanajeshi wa Kizayuni wameangamizwa na askari wake wengine 12,000 kulemazwa na wengine wengi kujeruhiwa kwa njia tofauti.

Mhimili mwingine katika hotuba ya Seyyid Hassan Nasrallah ni hatua ya utawala wa kibaguzi wa Israel ya kuficha ukweli kuhusu vita vya Ukanda wa Gaza. Ijapokuwa utawala wa Kizayuni umekuwa ukielezea hasara za kibinadamu na mali ulizopata katika kipindi cha miezi 3 iliyopita, lakini haujakuwa ukitoa takwimu sahihi kuhusiana na jambo hilo.

Baada ya kutaja takwimu za majeruhi wa utawala wa Kizayuni katika vita hivyo, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: "Kutotangaza idadi halisi ya majeruhi ni sehemu ya vita vya kisaikolojia vya adui ili kuficha fedheha na aibu yake mbele ya jamii, kwa sababu yanayojiri katika medani ya vita ni fedheha halisi na kushindwa Israeli katika mapambano ya kusini mwa Lebanon.

Mhimili wa tatu ni sisitizo lake kuhusu uwezo na nguvu ya wanamuqawana ya kuzuia kusonga mbele askari jeshi vamizi wa utawala unaoukalia kwa mabavu Quds Tukufu. Katika kipindi cha miezi 3 iliyopita, baadhi ya wapinzani wa harakati za wanamuqawama wamekuwa wakidai kwamba mapambano ya makundi hayo hayana itibari na athari yake haijauguza utawala huo kutokana na jinai zake kubwa na za wazi katika uwanja huo.

342/