Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Januari 2024

18:18:49
1427473

Daesh; Wakala wa niaba wa Marekani na utawala wa Kizayuni katika eneo

Kundi la kigaidi la Daesh Alhamisi usiku lilitangaza kuhusika na miripuko ya kigaidi katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa Iran huku genge hilo likihesabiwa kuwa kundi lililoasisiwa kwa niaba ya Marekani na utawala wa Kizayuni katika eneo la Asia Magharibi.

Mamia ya wananchi wa Iran waliuawa shahidi na kujeruhiwa alasiri ya Jumatano iliyopita katika hujuma ya miripuko miwili ya kigaidi iliyotekelezwa wakati wananchi walipokuwa katika marasimu ya kumbukumbu ya mwaka wa nne tangu kuuliwa kigaidi Shahidi Haj Qassim Suleiman aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH). Miripuko hiyo ilitekelezwa katika njia inayoekelea katika maziara ya Mashahidi wa mji wa Kerman.  Tangu awali, utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake yaani Marekani wanatambuliwa kuwa watuhumiwa nambari moja wa shambulio hilo la kigaidi huko Kerman kwa kuzingatia hali ya mambo ya eneo la Asia Magharibi khususan vita vinavyoendelea huko Gaza, kipigo na hasara kubwa iliyoupata utawala wa Kizayuni kutoka kwa muqawama wa Palestina. Hata hivyo Marekani na utawala wa Kizayuni kama ilivyokuwa huko nyuma zimekana kuhusika na jinai hiyo. Kwa mfano, Matthew Miller Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani amedai kuhusu tukio la ugaidi huko Kerman kuwa: "Washington haihusiki hata kidogo na miripuko ya Iran, na hakuna sababu ya kuamini kuwa Israel ilihusika." Naye Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni pia alisema katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano usiku kwamba: "Hatuna mjadala kuhusu miripuko ya Iran, na lengo letu ni kujielekeza katika vita dhidi ya Hamas." 

Hata hivyo ukweli wa mambo ni kuwa kundi moja la kigaidi kama Daesh kamwe haliwezi kufanya uhalifu kama huo bila ya msaada ulioratibiwa wa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.  

Ushahidi wa kweli unaonyesha kuwa, Marekani imehusika pakubwa katika kuasisi na kuliendeleza kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) ili kukabiliana na mhimili wa muqawama; na ilifanya juhudi endelevu za kupanua harakati za Daesh huko Iraq na Syria na kisha huko Afghanistan. Marekani ikiwa kinara wa nchi za Magharibi, pamoja na waitifaki wake wa Kiarabu imewaunga mkono pakubwa magaidi wa kitakfiri wakiwemo magaidi wa Daesh; huku ikiwatumia magaidi hao kama wenzo wa kufanikisha malengo yake haramu katika eneo. Donald Trump Rais wa zamani wa Marekani alisema katika mojawapo ya hotuba zake wakati wa uchaguzi mwezi Agosti 2016 katika duru ya urais wa Barack Obama kwamba, Obama na Hillary Clinton mgombea wa wakati huo wa kiti cha urais wa chama cha Democrat na Waziri wa zamani wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kuwa ndio walioasisi Daesh.   

Aidha Robert F. Kennedy Junior mwanasiasa wa  Marekani ambaye ametangaza kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka huu nchini humo na anayeesabiwa kuwa mpinzani wa Joe Biden katika chama cha Democrat amekiri juu ya kuhusika Marekani katika kuundwa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).



342/