Brigedia Jenerali Esmail Qaani ameyasema hayo katika ujumbe aliomtumia Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Saleh Al-Aouri, Naibu Mkuu wa ofisi hiyo ya kisiasa ya Hamas.Al-Arouri aliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi lililofanywa na utawala wa Kizayuni siku ya Jumanne katika viunga vya kusini mwa Beirut, mji mkuu wa Lebanon.Katika ujumbe wake huo kwa Haniya, Brigedia Jenerali Qaani, ametoa salamu za rambirambi kwa kuuawa shahidi Saleh al-Arouri na kueleza kuwa, adui Mzayuni anataka kupunguza uchungu wa kushindwa vibaya katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa kuwauwa viongozi wa Muqawama.Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Shahidi Al-Arouri aliuawa shahidi huku adui akikabiliwa na hali ngumu katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Al-Arouri ni mmoja wa waanzilishi wa Brigedi za Shahidi Izzuddin Al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Hamas, ambapo katika kipindi cha kati ya mwaka 1991-1992 alichukua hatua ya kuasisi kikosi cha kwanza cha tawi hilo la kijeshi la Hamas katika Ukingo wa Magharibi.Mwaka 1992, jeshi la utawala wa Kizayuni lilimkamata al-Arouri na kumhukumu kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kuunda kikosi cha kwanza cha Brigedi za Al-Qassam katika Ukingo wa Magharibi.
342/