Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Januari 2024

18:22:08
1427476

Ebrahim Raisi: Sera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kutetea madhulumu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, siasa za Iran ni kuwatetea na kuwalinda wanaodhulumiwa na kupaza sauti dhidi ya madhalimu.

Seyyed Ebrahim Raisi amesema hayo katika hadhara ya wananchi wa Zanjan jana (Jumamosi) ambapo sambamba na kulaani jinai ya kigaidi ya Kerman na kueleza kuwa siasa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni kuwatetea wanaodhulumiwa walimwengu na kupaza sauti  dhidi ya madhalimu na mabeberu amesema: Licha ya kuwepo njama za maadui katika nyuga tofauti, lakini taifa la Iran limesimama imara kwa kujitegemea lenyewe na litaibuka na ushindi.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria zaidi maendeleo ya Iran katika uga wa sayansi na teknolojia na kuongeza kuwa: Taifa la Iran limepiga hatua kubwa licha ya vikwazo na uadui na kuwaonyesha walimwengu kwamba, linaweza kuwa nchi iliyoendelea na ya kiteknolojia kwa kutegemea maadili na thamani za Kimungu, na hii leo, Iran ni nchi ambayyo iko namna hii duniani.Raisi ameashiria matukio ya Gaza na kusema: Uadui dhidi ya taifa la Iran na Shahidi Soleimani ni kwa sababu mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, taifa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu unatilia mkazo haki za Palestina na haki za wanyonge. Sambamba na kubainisha kwamba, batili ni yenye kuondoka, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Palestina inayodhulumiwa ina nguvu na utawala bandia wa Kizayuni lazima uondoke na uangamizwe.

342/