Main Title

source : Parstoday
Jumanne

9 Januari 2024

17:13:25
1428017

Kikundi cha Ushauri: Uchaguzi wa 2024 wa Marekani ndio hatari kubwa zaidi kwa dunia

Kundi la Ushauri la Uchambuzi wa Hatari la Eurasia limesema kuwa uchaguzi wa rais wa Marekani utaleta hatari kubwa zaidi ya kisiasa kwa ulimwengu katika mwaka huu wa 2024, bila kujali nani atashinda, kutokana na matumizi mabaya ya taasisi za demokrasia yenye nguvu zaidi duniani.

Katika ripoti yake ya kila mwaka iliyotolewa jana, Jumatatu, Tasisi ya Uchambuzi wa Hatari za Kisiasa ilisema kwamba uchaguzi wa rais wa Novemba 5, 2024 "utaijaribu demokrasia ya Marekani kwa kiwango ambacho taifa hilo halijashuhudia kwa miaka 150," ikiashiria vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Imeongeza kuwa: "Marekani tayari ndiyo nchi yenye demokrasia ya kiviwanda iliyogawanyika zaidi na isiyofanya kazi vyema zaidi duniani na uchaguzi wa 2024 utazidisha tatizo hili bila kujali nani atashinda."

Ripoti hiyo imesema kwamba iwapo Donald Trump, ambaye kwa sasa kuna uwezekano mkubwa kwamba atakuwa mgombea wa chama cha Republican, atashindwa tena na Rais wa sasa Joe Biden, bilionea huyo atadai tena kwamba kumefanyika udanganyifu mkubwa na "kuchochea kampeni za vitisho dhidi ya maafisa na wasimamizi wa uchaguzi." Ripoti hiyo imeongeza kuwa, iwapo Biden atashinda muhula wa pili, Merekani inaweza pia kukabiliwa na "mgogoro wa kisiasa ambao haujawahi kutokea" kama Donald Trump atafungwa jela katika mojawapo ya kesi nyingi zinazomkabili. Na iwapo Trump atashinda, kundi hilo linatarajia kwamba, Biden atakubali kushindwa, lakini Wademokrati wengi pia watamuona Trump kama kiongozi asiye halali, na wengine watakataa kuthibitisha ushindi wake, wakitegemea vifungu vya Katiba, ambavyo vinakataza mtu yeyote "anayeshiriki katika uasi" kushika nafasi hiyo. 

342/