Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Januari 2024

15:42:43
1428761

Shambulio dhidi ya Yemen, duru mpya ya chokochoko za Marekani na Magharibi katika eneo

Siku moja baada ya kupitishwa rasimu ya azimio lililopendekezwa na Marekani la kulaani kile kilichoitwa mashambulio ya Yemen dhidi ya meli katika Bahari Nyekundu, Washington imeishambulia Yemen katika duru mpya ya chokochoko zake katika eneo.

Siku ya Alhamisi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, bila ya kujali sababu zinazopelekea kufanyika mashambulizi ya Ansarullah ya Yemen katika Bahari Nyekundu na uungaji mkono wa Washington kwa utawala haramu wa Israel unaoendelea kutekeleza jinai za kutisha dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza, lilipitisha azimio nambari 2722 lililopendekezwa na Marekani kwa kura 11 za wajumbe wake wote 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa njia hiyo, ilitabiriwa tangu mwanzo kwamba Marekani kwa ushirikiano wa mshirika wake wa kawaida, Uingereza, imeandaa mazingira ya kuishambulia Yemen.

Kwa mujibu wa ripoti, na ikiwa ni katika kukabiliana na hujuma za anga na majini za Marekani na Uingereza, Jeshi la Taifa la Yemen leo limelenga kwa makombora maeneo na maslahi kadhaa ya Marekani na Uingereza katika Bahari Nyekundu. Saa chache baada ya Marekani na Uingereza kushambulia Yemen, bei ya mafuta duniani imeongezeka kwa asilimia 2.5.Mashambulizi mapya ya Marekani na nchi za Magharibi dhidi ya Yemen kwa kisingizio cha mashambulizi ya Ansarullah dhidi ya meli katika Bahari Nyekundu, yanafanyika katika hali ambayo Wayemen wamesisitiza mara kadhaa kwamba wanazilenga meli za Israel pekee au zile zinazoelekea kwenye bandari za Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) ikiwa ni katika kuliunga mkono taifa la Palestina na kushinikiza mashambulizi yanayofanywa na Wazayuni dhidi ya Wapaelestina wasio na hatia yasimamishwe mara moja.

Kuhusu mashambulizi ya kichokozi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen, Nasser Kanani, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani mashambulizi hayo na kuyataja kuwa ni hatua ya kujichukulia sheria mkononi na ukiukaji wa wazi wa mamlaka na umoja wa ardhi ya Yemen.


342/