Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Januari 2024

15:44:02
1428765

Abu Turabi Fard: Leo Yemen inaungwa mkono kila upande; Ghaza haishindiki

Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa Tehran amesema kuwa, leo hii Yemen shujaa inaungwa mkono kila upande na kwamba licha ya kupita siku 100 tangu utawala wa Kizayuni uanzishe jinai zake kila upande lakini imeshindwa kufikia malengo yake huko Ghaza.

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Mohammad Hossein Abu Turabi Fard amesema hayo na kuongeza kuwa, Msemaji wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa naye amekiri kwamba muqawama wa Ghaza haushindiki kwani ni aiodolojia madhubuti na hii ina maana ya kukiri rasmi kushindwa Marekani, utawala wa Kizayuni na madola ya Magharibi kwenye vita vya Ghaza.

Hayo yamekuja baada ya komandi ya jeshi la anga la Marekani kusema kuwa jeshi hilo limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya zaidi ya shabaha 60 na vituo 16 vya kijeshi vya Yemen kwa kutumia makombora 100 ya kuongozwa kwa mbali. 

Kwa upande wake jeshi la Yemen limesema kuwa, Marekani na Uingereza zimefanya mashambulizi 73 leo alfajiri dhidi ya mikoa tofauti ya Yemen na kuahidi kutoa majibu makali kwa mabeberu hao.Baada ya tamko hilo la jeshi la Yemen, Baraza la Kisiasa la Serikali ya San'a nalo limetoa taarifa na kusema kuwa, popole yalipo maslahi ya Marekani na Uingereza ni shabaha halali ya Yemen katika majibu yake makali yatakayokuja dhidi ya madola hayo ya kiistikbari. Shirika la habari la IRIB limemnukuu Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Mohammad Hossein Abu Turabi Fard akilaani mashambulizi hayo ya leo ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen na kusema kuwa, mashujaa wa Yemen lazima watatoa somo kali kwa mabeberu hao wa dunia. Vile vile amesema, kadhia ya Ghaza ndilo suala muhimu zaidi hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba siku 100 zimepita tangu Marekani na utawala wa Kizayuni zianze kufanya jinai kubwa dhidi ya watu wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan tena katika dunia hii ambayo inadaiwa imestaarabika. Lakini wenye fikra huru duniani wataendelea kuwa pamoja na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.

342/