Main Title

source : Parstoday
Jumanne

16 Januari 2024

18:34:46
1429962

Kiongozi Muadhamu: Watu waliodhulumiwa wa Gaza wameweza kuathiri ulimwengu kwa mapambano yao

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika kikao cha maimamu wa Swala za Ijumaa kote Iran kuwa: Watu madhulumu na wenye nguvu wa Gaza wameweza kuwaathiri walimwengu kwa mapambano yao.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ​​(Jumanne) katika kikao cha maimamu wa Swala za Ijumaa kote nchini Iran amesisitiza kwamba, leo mkono wa Mwenyezi Mungu unaonekana kufuatia kuchukua muelekeo wa kimataifa kadhia ya Gaza. Ameongeza kuwa: Leo hii dunia inawatazama watu wa Gaza, wanamapambano na makundi ya Muqawama kama mashujaa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutaja kupata umashuhuri  watu wanaodhulumiwa wa Gaza na wakati huo huo  ushindi mbele ya walimwengu kuwa ni kazi na baraka za subira na imani yao na kuongeza kuwa: Katika upande mwingine, leo hii,  hakuna mtu duniani anayeamini kwamba utawala ghasibu na khabithi wa Kizayuni umepata ushindi katika vita. Kwa maoni ya watu wa dunia na wanasiasa, utawala huo ni dhalimu, usio na huruma mbwa-mwitu mfyonza damu aliyeshindwa na kusambaratika.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, watu wa Gaza, kwa kusimama kidete, wameeneza Uislamu na mafundisho ya Qur'ani Tukufu mbele ya watu wanaotaka kujua ukweli duniani. Amemuomba Mwenyezi Mungu aongeze fahari ya wapiganaji walio mstari wa mbele wa mapambano hususan watu na wapiganaji wa Gaza.Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amepongeza kazi kubwa ya taifa la Yemen na serikali ya Harakati ya Ansarullah katika kuwaunga mkono wananchi wa Gaza na kubainisha kwamba, Wayemen walizigonga njia muhimu za utawala wa Kizayuni na hawakuwa na hofu kufuatia tishio la Marekani kwa sababu mcha Mungu haogopi chochote isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hatua waliyochukua kiuhakika ni mfano wa wazi wa Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Ayatullah Khamenei ameendelea kwa kueleza matumaini yake kuwa: "Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, mapambano, muqawama na harakati hizi zitaendelea hadi ushindi." Vilevile Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria uchaguzi ujao wa Iran na kutaja "mahudhurio, hamu na hatua ya watu" kuwa ni kanuni ya msingi katika Uislamu. Aidha amepongeza uaminifu, subira, busara na kujitolea kwa wananchi wa Iran. Ayatullah Khamenei halikadhalika amesema kushiriki katika uchaguzi ujao nchini ni wajibu na haki ya wananchi na kuongeza kuwa, ushiriki wa wananchi katika uchaguzi huo ni jambo la lazima kwa maana halisi ya neno hilo. Bila shaka, ameendelea kusema, uchaguzi si wajibu tu, bali ni haki ya wananchi kuwa na uwezo wa kuchagua wabunge, watekelezaji wa sheria au wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu.

342/