Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

19 Januari 2024

16:00:21
1430595

Mitazamo inayokinzana ya utawala wa Biden kuhusu Ansarullah ya Yemen

Sera na mienendo ya hivi karibuni ya serikali ya Joe Biden kuhusu harakati ya Ansarullah ya Yemen inaonyesha kusanganyikiwa kwa serikali ya Washington

Serikali ya Biden inatimiza karibu miaka mitatu ikwia madarakani. Siasa zinazokinzana za Marekani kuhusiana na harakati ya  Ansarullah ya Yemen zinaonyesha kuchanganyikiwa kwa Washington kuhusiana na harakati hiyo ya Yemen. Kwa upande mmoja, Washington inadai kutetea haki za binadamu za Ansarullah ya Yemen, na kwa upande mwingine, inawatambua Ansarallah kuwa ni magaidi na inachukua hatua za kijeshi dhidi yao kwa sababu tu ya maslahi ya Wazayuni. Hadi sasa serikali ya Biden imekuwa na mienendo na mitazamo ya aina tatu tofauti kuhusiana na kundi la Ansurallah la Yemen.Mwenendo wa kwanza ulichukuliwa mwanzoni mwa utawala wa Biden ambapo jina la Ansarullah liliondolewa kwenye orodha ya magaidi. Serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani iliondoa jina la harakati ya Ansarullah ya Yemen katika orodha ya makundi ya kigaidi mwezi Februari 2021. Taarifa  iliyochapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Fedha ya Marekani ilieleza kuwa: Sheria ya kuiweka harakati ya Ansarullah ya Yemen katika orodha ya makundi ya kigaidi imefutwa kuanzia tarehe 16 Februari 2021 na kutokana na mabadiliko yaliyofanyika, harakati hiyo haitakuwa tena chini ya sheria za vikwazo za ugaidi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken, pia alitangaza tarehe 16 Februari  2021 kwamba kwa kuzingatia masuala ya kibinadamu na haja ya kutumwa misaada ya kibinadamu katika nchi iliyokumbwa na vita na mgogoro ya Yemen, harakati ya Ansarullah imeondolewa katika orodha ya mashirika ya kigaidi ya nchi hiyo.

Mwenendo wa pili ni ule wa hivi karibuni unaohusiana na vita vya Gaza. Katika kipindi cha wiki zilizopita Wayemeni wamezishambulia mara kadhaa meli za Israel au meli yoyote inayoelekea Israel. Wayemeni walichukua hatua hiyo kwa lengo la kuwatetea watu wa Gaza na kwa ajili ya kukomesha mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina. Ijumaa iliyopita, Marekani na Uingereza zililenga baadhi ya maeneo ya Yemen kwa lengo la kusimamisha mashambulizi ya Ansarullah na jeshi la Yemen dhidi ya meli zinazopeleka bidhaa huko Israel. Mashambulizi hayo yalikaririwa katika siku zilizofuata, lakini Serikali ya Wokovu wa Kitaifa yenye makao yake makuu mjini Sana'a, mji mkuu wa Yemen, ilitangaza kwamba itaendeleza mashambulizi dhidi ya meli zinazoelekea Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Katika mwendelezo wa hali hiyo, Rais Joe Biden wa Marekani aliitaja harakati hiyo kuwa ni kundi la kigaidi baada ya kushambulia maeneo ya Ansarullah. 

Matamshi ya Biden yanakuja wakati John Kirby, mratibu wa mawasiliano ya kimkakati katika Baraza la Usalama wa Taifa la Ikulu ya White House (Jumanne, Disemba 28), alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba Marekani inachunguza hali ya harakati ya Ansarullah nchini Yemen, lakini bado haijafanya uamuzi wa kuitangaza kuwa ni kundi la magaidi.



342/