Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

20 Januari 2024

19:20:54
1430956

New York Times: Iran imetuma ujumbe kwa Israel kwa kombora la Khaybar-Shekan

Gazeti la Marekani la New York Times limelitaja shambulio la hivi karibuni la makombora ya Iran dhidi ya ngome za kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) nchini Syria kwa kutumia kombora la kisasa la "Khaybar Shekan" kuwa sio tu ni kulipiza kisasi dhidi ya ISIS bali pia ni onyesho la nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya kambi ya Magharibi na hasa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mapema Jumanne iliyopita, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, lilishambulia maeneo ya mikusanyiko ya makamanda na wakuu operesheni za hivi karibuni za makundi ya kigaidi hususan ISIS katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu nchini Syria kwa makombora kadhaa ya balestiki, yakiwemo makombora 4 ya "Khaybar Shekan". Shambulizi hilo lilifanyika kujibu jinai zilizofanywa hivi karibuni na makundi ya kigaidi katika miji ya Kerman na Rask, kusini mwa Iran.Gazeti la New York Times limeandika kuhusu suala hilo kwamba: Iran ilitumia moja ya makombora yake ya masafa marefu na ya kisasa zaidi liitwalo "Khaybar Shekan" katika shambulio dhidi ya magaidi wa ISIS. Masafa na usahihi wa kulenga shabaha wa kombora la "Khaybar Shekan" vimepewa mazingatio maalumu na maafisa wa usalama barani Ulaya na Israel, pamoja na wataalamu wanaofuatilia maendeleo ya kiteknolojia ya Iran. Gazeti la Marekani la New York Times limeandika kuwa, mchanganyiko wa makombora ya kisasa na ndege zisizo na rubani umeisaidia Iran kuwa mzalishaji wa baadhi ya silaha tata zaidi katika eneo la Asia Magharibi, na uwezo wake wa kuzalisha maelfu ya ndege zisizo na rubani umewashangaza maafisa wengi wa nchi za Magharibi. Kombora la Khaybar Shekan, lililozinduliwa mwaka wa 2022, ni kombora linaloongozwa na fueli mango na linaweza kupiga shabaha umbali wa kilomita 1,450. Miongoni mwa sifa za kipekee zinazotofautisha kombora la Khaybar Shekan na makombora mengine ya Irani ni kichwa chake ambacho huruka kwa kutumia mbawa za aerodynamic na kukwepa baadhi ya mifumo ya ulinzi wa anga.

342/