Main Title

source : Parstoday
Jumapili

21 Januari 2024

15:56:56
1431270

Amir-Abdollahian: Harakati za washauri wa kijeshi wa Iran za kupambana na ugaidi zitaendelea kwa nguvu kamili

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa mjibizo kufuatia kuuawa shahidi washauri watano wa Iran nchini Syria katika shambulio la kigaidi la utawala wa Kizayuni na kueleza kwamba: "kushindwa Wazayuni kukabiliana na irada na matakwa ya watu wa Gaza hakutaweza kufidiwa kwa vitendo hivi vya kigaidi."

Kufuatia shambulio lililofanywa na ndege za kivita za  utawala wa Kizayuni mjini Damascus jana Jumamosi asubuhi, washauri watano wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na walinzi wa Haram waliuawa shahidi na wengine kadhaa walijeruhiwa.

Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa mjibizo kupitia mtandao wa kijamii wa X kwa hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni ya kuishambulia kijeshi Syria na kuwaua washauri wa kijeshi wa Iran akisisitiza azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kupambana na ugaidi na kuhakikisha eneo linakuwa na amani na usalama na kuandika kuwa: "harakati za washauri wa kijeshi wa Iran katika kupambana na ugaidi na kuhakikisha eneo linakuwa na usalama zitaendelea kwa nguvu kamili."
Amir-Abdollahian ameashiria hatua za Wazayuni za kuzusha taharuki na mivutano katika eneo na namna wanavyoendelea kuchezea kipigo cha muqawama wa Palestina katika medani ya mapigano na akasema: utawala wa Israel ni mshirika mkuu wa harakati za kigaidi na adui namba moja wa usalama wa eneo. Hakuna shaka kuwa kushindwa Wazayuni kukabiliana na irada na matakwa ya watu wa Palestina hakutaweza kufidiwa kwa vitendo vya kutapatapa vya kigaidi."Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran naye pia amezungumzia ugaidi wa Wazayuni wa kulishambulia eneo la Zainabiyah mjini Damascus na kuwaua shahidi washauri wa Kiiran na akasema: "hapana shaka kuendelea kwa hatua za aina hii za kigaidi na za kijinai, ambazo zinatokana na kuendelea kushindwa kila uchao utawala haramu wa Kizayuni katika kufikia malengo yake maovu na kufikia hatua ya kukata tamaa na kuchanganyikiwa katika kukabiliana na wapiganaji wa muqawama, hakutaachwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bila ya kujibiwa".

Baada ya utawala haramu wa Kizayuni kushindwa kufikia malengo yake ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza, sasa umegeukia mbinu ya kuwaua makamanda wa muqawama.
Katika wiki za hivi karibuni, utawala wa Kizayuni na kwa usaidizi na uungaji mkono wa Marekani, umefanya operesheni kadhaa za kigaidi kuwalenga makamanda wa Mhimili wa Muqawama, ambapo Sayed Razi Mousavi, mmoja wa makamanda wa Iran nchini Syria, Wissam At-T'awil, mkuu wa operesheni za kijeshi za Hizbullah ya Lebanon na Saleh Al-Arouri, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, ni miongoni mwa makamanda wa Muqawama waliouawa shahidi katika mashambulizi ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni.../



342/