Main Title

source : Parstoday
Jumapili

21 Januari 2024

15:57:20
1431271

Sayyid Nasrullah: Gaza ni nembo ya umoja wa damu, silaha, medani na lengo la Umma wa Kiislamu

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah ametuma ujumbe katika Mkutano wa 12 wa Kimataifa wa "Gaza; Nembo ya Muqawama" na kusisitiza kuwa Gaza leo hii ni nembo ya umoja wa damu, silaha, medani na lengo la Umma wa Kiislamu.

Mkutano wa 12 wa Kimataifa wa Gaza Nembo ya Muqawama ulifanyika jana Tehran ukihudhuriwa na familia za mashahidi wa Muqawama, viongozi kadhaa wa serikali ya Iran na wageni kutoka kambi ya kimataifa ya Mapambano.  

Shirika la habari la TASNIM limeripoti kuwa, Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema katika ujumbe wake huo kuwa, operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa imeacha alama ya kushindwa katika fikra za Wazayuni na kwamba operesheni hiyo ilitoa kipigo kikubwa kwa jitihada zote zilizokuwa na lengo la kuyaweka kando malengo ya ukombozi wa Palestina.Sayyid Nasrullah ameongeza kuwa: Gaza ni nembo kwa sababu kuna katika eneo hilo kuna mapambano matakatifu yasiyokubali kufanya mapatano ya Wazayubi maghasibu. Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amashiria pia mashahidi wa Muqawama na kusema: Damu ya mashahidi walanaouliwa katika kuitetea Gaza huko Iran, Lebanon, Syria, Iraqi na Yemen; damu zote hizi zimetengeneza umoja na mshikamano na damu ya mashahidi wa Ukaknda wa Gaza na wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kukamilishana. Wakati huo huo, Ebrahim Al-Dailami Balozi wa Yemen mjini Tehran amesema katika mkutano huo wa Tehran kwamba Wamarekani hawana uwezo wa kukabiliana na mhimili wa Muqawama na kwamba, muungano na mshikamano wa mhimili wa Muqawama katika kalibu ya kutetea Msikiti wa Al-Aqswa umejitokeza wakati wa Kimbunga cha Al-Aqsa. 

342/