Main Title

source : Parstoday
Jumapili

21 Januari 2024

15:58:47
1431274

Marekani: Israel imeshindwa kufikia lengo la vita, HAMAS ingali iko imara, ina silaha za kutosha

Mashirika ya intelijensia ya Marekani yamesema, idadi ya vifo vya wapiganaji wa harakati ya HAMAS vilivyotokana na uvamizi unaoendelea wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza haifikii lengo la utawala huo la kulitokomeza kundi hilo la muqawama wa Palestina.

Kwa mujibu wa gazeti la Wall Street, katika ripoti yao ya siri, mashirika ya kiintelijensia ya Marekani yaliyoangazia uthabiti wa Hamas katika miezi iliyopita yamesema vita vya Israel vimeua asilimia 20 hadi 30 tu ya wanachama wa harakati hiyo ya Muqawama.

Maafisa wa Marekani ambao wamethibitisha kutolewa kwa ripoti hiyo na kusema: "Hamas ingali ina silaha za kutosha kuweza kuendelea kushambulia Israel na vikosi vya Israel huko Gaza kwa miezi kadhaa, na kundi hilo linajaribu kuunda upya jeshi lake la polisi katika maeneo ya mji wa Gaza".

Ripoti hiyo imeendelea kufichua kwamba, maafisa wenyewe wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamekiri kwamba hawajafikia lengo lao la kuiangamiza Hamas licha ya kuua maelfu ya raia katika mashambulio ya kinyama ya anga na ardhini yaliyofanywa na jeshi lake huko Gaza.

342/