Main Title

source : Parstoday
Jumapili

21 Januari 2024

15:59:39
1431276

Kan'ani: Kuna uhusiano mkubwa kati ya utawala gaidi wa Israel na Daesh

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali jinai na uchokozi uliofanywa mapema jana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la raia huko al Mezza, Damascus mji mkuu wa Syria na kuuwa shahidi washauri watano wa kijeshi wa Iran na askari kadhaa wa Syria.

Nasser Kan'ani jana alasiri alilaani jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni na kuitaja kuwa inakiuka mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Syria.

Kanani ameongeza kuwa hatua hiyo ya kichokozi ya utawala ghasibu wa Israel inadhihirisha udhaifu na kushindwa utawala huo ghasibu katika medani ya vita mkabala wa vikosi vya muqawama huko Gaza na katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katika kipindi cha zaid ya siku 100; na wakati huo huo hujuma hiyo inabainisha namna utawala wa Kizayuni unavyojaribu kila linalowezekana  kueneza ukosefu wa amani na utulivu katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameitolea wito serikali na taasisi za kikanda na kimataifa likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutoa radiamali na jibu la haraka kwa mashambulizi, vitendo vya kigaidi na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na kulaani vikali hujuma hizo.

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa, mauaji ya washauri wa kijeshi wa Iran yaliyyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel yanaonyesha wazi uhusiano wa kina na uliopangwa kati ya utawala huo wa kigaidi na makundi mbalimbali ya kigaidi kama ISIS katika eneo la Asia Magharibi. 

Mwishoni Kan'ani ameeleza kuwa damu za mashahidi hao wa ngazi za juu hazitapotea bure na kuongeza kuwa: Sambamba na kufuatilia suala hilo kisiasa, kisheria na kimataifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalinda haki yake ya kutoa jibu kwa ugaidi uliopangwa wa utawala bandia wa Israel katika wakati na mahali mwafaka.

342/