Main Title

source : Parstoday
Jumanne

23 Januari 2024

14:44:57
1431834

Kiongozi Muadhamu: Kuna udharura wa kukatwa mishipa ya uhai ya utawala wa Kizayuni

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Nchi za Kiislamu zinapaswa kukata uhusiano wao wa kisiasa na kiuchumi na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kukata mishipa muhimu ya uhai ya utawala huo ghasibu.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei amekosoa utendaji wa viongozi wa nchi za Kiislamu kuhusiana na suala muhimu sana la Gaza na kusema: "Wakati fulani misimamo na matamshi ya viongozi hao nchi za Kiislamu ni makosa kwa sababu wanazungumzia suala kama vile usitishaji vita huko Gaza, ambalo liko nje ya uwezo wao na liko chini ya udhibiti wa adui muovu wa Kizayuni."

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa: Licha ya utendaji usiofaa wa viongozi wa nchi za Kiislamu na licha ya matatizo yote yaliyopo, tunasoma katika Qur'ani Tukufu kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja na watu wenye imani thabiti na popote pale alipo Mwenyezi Mungu kutakuwa na ushindi.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Ushindi wa watu wa Gaza ni wa uhakika, na Mwenyezi Mungu Mtukufu atauonyesha Umma wa Kiislamu ushindi huo katika mustakabali usio mbali, na nyoyo za Waislamu hususan watu wa Palestina na Gaza, zitafurahishwa na ushindi huo.

342/