Main Title

source : Parstoday
Jumanne

23 Januari 2024

14:47:04
1431838

Mkuu wa Intelijensia ya Russia: Marekani inaanzisha 'Serikali ya Kikoloni' ndani ya Ukraine

Mkuu wa Shirika la Intelijensia la Russia amesema, Marekani imeanza kuunda "serikali ya kikoloni" nchini Ukraine inayojumuisha wanasiasa wa ndani ambao wamekula kiapo cha utiifu kwa Washington.

Sergey Naryshkin amefafanua kuwa, serikali ya Marekani imemtaka Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskky "kuondoa" makumi ya maafisa wa ngazi za juu, ambao Washington haiwaamini tena katika nyadhifa zao kwa visingizio mbalimbali.

Naryshkin ameongeza kuwa, Washington inataka nafasi hizo za uongozi zijazwe na "Waukraine waliosomeshwa Magharibi, ambao wameapa kuonyesha utiifu kwa maslahi ya Marekani".

Mkuu huyo wa shirika la intelijensia la Russia amesisitiza kuwa, ikiwa ni sehemu ya sera ya uvamizi kamili wa ardhi ya Ukraine, Marekani imeanza kuunda kile ambacho kimsingi ni utawala wa kikoloni katika nchi hiyo.

342/