Main Title

source : Parstoday
Jumatano

24 Januari 2024

19:30:04
1432137

Kugunduliwa makaburi ya halaiki ya watu weusi huko Florida Marekani, ukumbusho wa mateso ya kihistoria

Ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wa watu wasio wazungu, haswa watu weusi, huko Marekani ni wa siku nyingi kama historia ya nchi hiyo. Kuhusiana na jambo hilo, Jeshi la Wanahewa la Marekani limetangaza kugundua makaburi 121 ya watu weusi katika Kituo cha Jeshi la Anga cha MacDill huko Tampa.

Luteni Laura Anderson, mmoja wa maafisa wa Jeshi la Anga la Marekani, ametangaza kuwa, kugunduliwa kwa makaburi hayo ya umati kumekuja baada ya uchunguzi uliofanywa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika Kambi ya Jeshi la Anga ya MacDill huko Tampa, na kwamba uchunguzi wa kubaini undani wa kadhia hii bado unaendelea.

Ubaguzi wa rangi na watu wasiokuwa wazungu daima umekuwa mojawapo ya sifa kuu za jamii ya Marekani, na watu weusi wamekuwa waathiriwa zaidi katika historia ya nchi hiyo; kwa kadiri kwamba historia ya Marekani ina faili chafu ya kipindi cha utumwa na unyanyasaji mkubwa wa watu weusi. Hata harakati ya kutetea haki za kiraia za watu weusi iliyoanzishwa miaka 1950 ambayo iliamsha wimbi la kutetea haki zao na kupinga ubaguzi wa rangi,  haikufanikiwa katika suala hilo la kuwepo usawa nchini humo.Ingawa mamlaka za Marekani zimejaribu katika miongo ya hivi karibuni kuwachukulia watu weusi kama raia sawa na wazungu na kuzungumzia suala la kutokomeza ubaguzi na unyanyasaji dhidi ya watu wenye asili ya Afrika, lakini vielelezo vya kihistoria na utendaji wa sasa wa mamlaka ya Marekani vinaonyesha kuwa watu weusi wachache ndio wanaoteseka zaidi kutokana na ubaguzi na unyanyasaji.

Kwa hakika, weusi wengi wenye asili ya Kiafrika katika jamii ya Marekani wanabaguliwa na kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa wazi katika sekta tofauti za kijamii, kiuchumi, kiafya na hata katika nyanja za kielimu. Wengi wao wanaishi katika maeneo ya kimaskini na duni, na isiyokuwa na huduma za kijamii na kubaguliwa katika ajira na kiwango cha mishahara ikilinganishwa na wazungu,  suala ambalo limechangia kuongeza sana kiwango cha vifo baina yao.

Katika muktadha huo, moja ya tafiti zilizochapishwa hivi karibuni katika jarida la Jumuiya ya Madaktari ya Marekani umeonyesha kwamba, kiwango cha vifo vya watu weusi nchini Marekani kimekuwa cha juu zaidi ikilinganishwa cha wazungu katika miongo miwili iliyopita.



342/