Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

25 Januari 2024

13:38:19
1432361

Seneta Sanders: Washington ni mshirika wa jinai za Israel huko Gaza

Seneta wa jimbo la Vermont nchini Marekani amesema serikali ya Washington ni mshirika katika jinai za kutisha za Israel huko Ukanda wa Gaza kutokana na uungaji mkono wake kwa utawala huo unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Bernie Sanders amesema hatua ya Marekani ya kuupa utawala dhalimu wa Israel misaada ya kijeshi na kilojistiki inaifanya Washington kuwa mshirika wa mauaji ya halaiki ya Wapalestina wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza.

Sanders amebainisha kuwa, Marekani inabeba dhima kwa mauaji ya kutisha yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya Wapalestina katika eneo lililozingirwa la Ukanda wa Gaza.

Sanders ameitaka serikali ya Marekani isimamishe misaada ya silaha inayotoa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel unazozitumia kuulia wananchi madhulumu wa Palestina.

"Tunapasa kutangaza msimamo wetu, Biden anapasa kupinga wazi wazi sera za baraza la mawaziri la (Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin) Netanyahu," amesisitiza Sanders na kuongeza kuwa: Iwapo Netanyahu anataka kuendelea na njia hii ya kuidhibiti kijeshi Gaza, lazima aachwe afanye hayo mwenyewe, hatupasi kuwa washirika wake.Mwezi uliopita wa Disemba pia, Seneta huyo wa kujitegemea wa Marekani, alimwandikia barua rais wa nchi hiyo Joe Biden akitaka kusitishwa msaada wa kijeshi kwa Israel kutokana na vita vya Gaza. Katika barua yake hiyo, Sanders aliandika, "mbali na vifo vingi, tunashuhudia watu wengi wakibaki bila makazi. Vita hivi sio janga la kibinadamu tu, lakini pia ni jinai na uhalifu mkubwa." Matokeo ya pamoja ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na CBS News na taasisi ya uchunguzaji maoni ya YuGov yanaonyesha kuwa asilimia 61 ya Wamarekani hawakubaliani na sera za Rais Joe Biden kuhusu vita vya Gaza. Seneta huyo wa jimbo la Vermont amesisitiza kuwa, Rais wa Marekani Joe Biden ni mshirika katika uhalifu wa mauaji ya kimbari yanayofanywa na Netanyahu dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

342/