Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

26 Januari 2024

15:50:09
1432561

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Utawala haramu wa Israel umeshindwa kufikia malengo yake Gaza

Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema: Utawala wa Kizayuni umeshindwa katika Ukanda wa Gaza na kwamba, haujafikia lengo lolote kati ya malengo yake.

Hujjatul Islam Wal-Muslimin Sheikh Muhammad Jawad Haj Ali Akbari amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa mjini Tehran ambapo amesisitiza kuwa, baada ya siku 110 tangu kutekelezwa operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa, habari zote zinaonyesha kushindwa kwa utawala ghasibu wa Israel na waungaji mkono wake hukku mujahidina na wananchi wa Palestina na Gaza wakiibuka na ushindi.

Huku akiashiria kwamba, utawala wa Kizayuni haujafikia malengo yake yoyote huko katikka Ukanda wa Gaza, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: "Wananchi wa Palestina wamesimama kidete na wameweza kuusababishia hasara na pigo kubwa utawala wa Kizayuni."Katika sehemu nyingine ya hotuba zake za Sala ya Ijumaa, Sheikh Haj Ali Akbari ameashiria uchaguzi ujao wa Bunge, Mabaraza ya Kiislamu na Jopo la Wanazuoni Wanamchagua Kiongozi Muadhamu hapa nchini unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni na kusisitiza kwamba, wananchi wa Iran kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi hizo watasambaratisha njama zote za maadui, kwani kushiriki katikak uchaguzi ni jukkumu la Kiislamu, kitaifa na la wote. Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria njama za maadui za kuutia dosari uchaguzi ujao na kusema kuwa, moja kati ya chaguzi salama zaidi ulimwengu ni uchaguzi unaofanyika katikka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

342/