Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

26 Januari 2024

15:50:34
1432562

Raisi: Uamuzi wa Afrika Kusini wa kuishtaki Israel unasifiwa na wapigania uhuru

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza yanapongezwa na kusifiwa na watu wote wanaopigania uhuru na ukombozi.

Rais wa Iran amesema hayo leo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na kueleza kwamba nia ya maafisa wa nchi hizo mbili ni kuboresha zaidi uhusiano katika nyanja mbalimbali.

Sambamba na kupongeza hatua hatua ya kijasiri ya serikali ya Afrika Kusini katika kuwasilisha shauri la mashtaka dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki amesema: Hatua hii inatoka kwa nchi ambayo imekumbwa na machungu ya ubaguzi wa rangi na mauaji ya kimbari kwa miaka mingi.

Aidha amesema, hatua hiii ya Afrika Kusini haisifiwi na kupongezwa tu katika ulimwengu wa Kiislamu bali katika mataifa yote ya ulimwengu ambayo yanapenda uhuru na haki.

342/