Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

26 Januari 2024

15:52:50
1432565

Mbunge Muislamu wa Uingereza amkosoa Waziri Mkuu wa nchi hiyo

Mbunge Muislamu katika bunge la Uingereza wa chama cha Labour amemkosoa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kuitaja serikali ya London kuwa inabeba dhima ya damu ya maelfu ya Wapalestina wasio na hatia.

Tahir Ali mwakilishi katika bunge la Uingereza anayekiwakilisha chama cha Labour amemkosoa Rish Sunak Waziri Mkuu wa nchi hiyo katika kikao cha serikali na wabunge kilichofanyika jana Alhamisi bungeni.

Tahir Ali ameeleza  kuwa: Waziri Mkuu huyo anadai kuwa utawala wa Kizayuni unaheshimu sheria za kimataifa katika hali ambayo jinai za kivita za utawala huo katika ukanda wa Gaza zimewabainikia wazi walimwengu huku Afrika Kusini ikiwa tayari imefungua kesi kuhusu jinai za Israel Ukanda wa Gaza katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ). 

Tahir Ali ambaye ni mbunge wa Birmingham wa chama cha Labour ameongeza kusema kuwa: "Je, wakati bado haujafika kwa Waziri Mkuu wa Uingereza kutaka kusitishwa haraka iwezekanavyo vita   katika Ukanda wa Gaza na kuhitimisha mauzo ya silaha ya Uingereza kwa utawala wa Kizayuni? 

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Uingereza amehutubu mbunge huyo wa Uingereza wa chama cha Labour kwamba: Hii ndio taswira ya chama cha Labour ambayo inapasa kubadilika. 

Zaidi ya miezi mitatu imepita sasa tangu utawala wa Kizayuni uanzishe mauaji makubwa na ya kikatili dhidi ya wakazi wa Kipalestina wa  Ukanda wa Gaza kwa  uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi. Serikali ya Uingereza imetangaza kuunga mkono kikamilifu utawala wa Kizayuni tangu utawala huo haramu uanzishe mashambulizi dhidi ya Gaza huku ikipuuza mauaji ya Wapalestina.

342/