Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

26 Januari 2024

15:53:29
1432566

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Poland waandamana kupinga uungaji mkono wa Ujerumani kwa Israel

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Warsaw nchini Polanda wameandamana kupinga uungaji mkono wa serikali ya Ujerumani kwa utawala wa Kizayuni.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Warsaw mji mkuu wa Poland wamelalamikia na kupinga uungaji mkono wa Ujerumani kwa utawala wa Kizayuni. Wanafunzi hao walimweleza Marco Buschmann Waziri wa Sheria wa Ujerumani ambaye alikuwepo katika Chuo hicho Kikuu cha Warsaw kwamba: Ni jambo lililo wazi kuwa utawala wa Kizayuni unakiuka sheria za kimataifa; hadi sasa utawala wa Israel umewauwa shahidi Wapalestina zaidi ya elfu 25 huku Ujerumani ikiendelea kuupatia utawala huo silaha mbalimbali.  Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Warsaw wamesema kuwa, Ujerumani inazuia maandamano ya kuiunga mkono Palestina katika hali ambayo utawala wa Kizayuni hadi sasa umeuwa watoto wa Kipalestian elfu kumi, umebomoa asilimia 60 ya nyumba za Ukanda wa Gaza na haujabakisha hata hospitali moja inayofanya kazi katika eneo. Hii ni katika hali ambayo zaidi ya asilimia 55 ya watu wa Gaza wanakabiliwa na njaa. Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Warsaw mji mkuu wa Poland wameongeza kuwa: Ujerumani inawanyima haki za raia wale wote wanaoiunga mkono Palestina, huku wapigania uhuru na ukombozi duniani wakijaribu kutumia mbinu na majukwaa mbalimbali kutangaza sauti zao za maandamano na kuunga mkono wananchi wa Palestina.

342/