Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini ilisema jana Alhamisi katika taarifa yake kuwa Naledi Pandor Waziri anayesimamia wizara hiyo anaongoza ujumbe wa nchi hiyo katika kikao cha kusikiliza uamuzi utakaotolewa na mahakama ya ICJ kuhusiana na kesi iliyowasilishwa na nchi hiyo kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza.
Afrika Kusini Disemba 29 mwaka jana iliwasilisha kesi katika mahakama ya ICJ ikiiomba mahakama hiyo iiamuru Israel isitishe mashambulizi yake dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza kwa misingi kwamba yanakiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari wa Umoja wa Mataifa.
Maombi ya Afrika Kusini kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu jinai za Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza ni kwamba inataka mahakama hiyo ichukue hatua za awali ikiwemo iiamuru Israel isitishe mara moja oparesheni za kijeshi huko Gaza, mahakama hiyo ichukue hatua za maana za kuzuia mauaj ya kimbari ya Wapalestina, ihakikishe Wapalestina waliokimbia makazi yao wanarejea huko Gaza na wanafikiwa na misaada ya kibinadamu kama chakula, maji, nishati huduma za matibabu n.k.
342/