Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

27 Januari 2024

18:17:34
1432920

Hukumu ya Mahakama ya The Hague; Nukta muhimu katika kutafuta haki kwa ajili ya watu wa Palestina

Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, yenye makao yake huko The Hague Uholanzi imetoa hukumu yake ya awali kwa shauri la mashtaka lililowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu mauaji ya kimbari ya utawala huo huko Ukanda wa Gaza.

Mwezi wa nne unapita sasa tangu utawala haramu wa Israel uanzishe vita dhidi ya watu wa Gaza. Wizara ya Afya ya Gaza jana Ijumaa ilitangaza kuwa hadi sasa Wapalestina 26,083 wameuliwa shahidi na wengine 64,487 wamejeruhiwa tangu kuanza vita vya utawala huo ghasibu Oktoba 7 mwaka jana.Afrika Kusini iliwasilisha mashtaka katika mahakama ya ICJ dhidi ya utawala wa Kizayuni baada ya kushtadi jinai za utawala huo huko Gaza na maangamizi ya kizazi yanayofanywa na Israel katika eneo hilo la Palestina. Kuna mambo kadhaa muhimu katika uamuzi wa awali uliotolewa jana na mahakama ya ICJ. 

Kwanza ni kwamba Israel iligonga mwamba kwa mara ya kwanza mbele ya mahakama hiyo kwa sababu ICJ ilikataa ombi la Israel kwamba haiafiki mashtaka ya Afrika Kusini dhidi yake. Mahakama ilitangaza kuwa ina mamlaka ya kushughulikia malalamiko hayo na kufafanua kuwa, Afrika Kusini ina haki ya kuishtaki Israel katika mahakama hiyo. Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imetangaza kuwa ripoti zilizowasilishwa na Afrika kusini ni za kimantiki na kwamba zinapaswa kuchunguzwa. 

Pili ni kwamba, Mahakama ya The Hague ilitoa uamuzi na kutangaza kuwa ina mamlaka ya kushughulikia kesi iliyofunguliwa na Afrika Kusini kuhusu mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Israel dhidi ya  Wapalestina wa Ukanda wa Gaza. Majaji 16 kati ya 17 wa mahakama hiyo wanaamini kuwa Israel inapaswa kukomesha vitendo vya mauaji ya halaiki na uharibifu katika Ukanda wa Gaza. Kwa msingi huo, ingawa mahakama ya ICJ imetangaza kuwa kkwa sasa haitatoa uamuzi kama mauaji ya halaiki yametokea au la, lakini suala la kujiri mauaji ya kimbari liko wazi kwa wajumbe wa mahakama hiyo, kwa sababu  muendelezo wa hukumu hiyo ya jana unaeleza kuwa: "Watu wa Palestina wana haki ya kuwa salama na mbali na mauaji ya kimbari." 


342/