Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

29 Januari 2024

14:36:00
1433497

Askari 3 wa Marekani wauawa, 30 wajeruhiwa Jordan; Muqawama wa Iraq wathibitisha kuhusika

Askari watatu wa jeshi la Marekani wameuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani kwenye kambi ndogo ya jeshi hilo iliyoko nchini Jordan.

Shambulio hilo lilitokea jana Jumapili katika eneo la Mnara wa 22 karibu na mpaka na Syria, likiwa ni tukio la kwanza la kuuawa wanajeshi wa Marekani katika eneo hili tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha vita na mauaji ya kinyama katika Ukanda wa Gaza mapema mwezi Oktoba. Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) imetoa taarifa ya kuthibitisha kuuawa wanajeshi hao na kujeruhiwa wengine 30 katika shambulio hilo la droni lililolenga "kambi moja kaskazini mashariki mwa Jordan." Afisa mmoja wa Marekani ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba askari wasiopungua 34 wanachunguzwa kuona kama pengine watakuwa wameathirika ubongo.Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq ya Kataaeb Hizbullah imetoa taarifa na kutangaza kwamba ndiyo iliyohusika na shambulio hilo la ndege zisizo na rubani kwenye kituo cha Al-Tanf kwenye mpaka wa Syria na Jordan.