Main Title

source : Parstoday
Jumanne

30 Januari 2024

19:45:38
1433829

Chama cha Labour Uingereza chamsimamisha kazi mbunge kwa kuyataja mashambulizi ya Israel huko Gaza kuwa ni ‘mauaji ya kimbari’

Chama cha Labour cha Uingereza kimemsimamisha kazi mbunge Kate Osamor baada ya kusema vita vya Israel dhidi ya Gaza vinapaswa kukumbukwa kama mfano wa mauaji ya kimbari duniani.

Osamor alituma ujumbe kwa wanachama wa chama chake siku ya Jumapili - mkesha wa Siku ya Kumbukumbu ya Holocaust - akiorodhesha Gaza miongoni mwa mifano ya hivi karibuni ya mauaji ya kimbari. Miongoni mwa mauaji ya kimbari yanayopaswa kukumbukwa duniani yaliyotajwa na mbunge huyo wa Uingereza ni yale yaliyofanyika Cambodia, Rwanda, Bosnia na sasa Gaza.

Maafisa wa chama cha Labour wamethibitisha kuwa Osamor amesimamishwa kazi na kiongozi wa upinzani, Sir Alan Campbell, "kusubiri uchunguzi."

Baraza la Wabunge Wayahudi la Uingereza limeshutumu kile lilichosema ni "jaribio la Kate Osamor la kuhusisha mauaji ya Holocaust na hali ya sasa huko Gaza," na kuyaeleza matamshi yake kuwa "ya kufedhehesha."

Itakumbukwa kuwa Afrika Kusini imewasilisha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ikiituhumu Israel kuwa inafanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina. Mashtaka hayo ya Afrika Kusini yameungwa mkono na nchi nyingi duniani. Uingereza, Marekani na nchi kadhaa wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekuwa zikiipatia Israel silaha na misaada ya kijeshi tangu utawala huo katili ulipoanzisha vita dhidi ya watu wa Gaza Oktoba 7, 2023. Hadi sasa Wapalestina zaidi ya elfu 26 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi hayo. 

342/