Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

1 Februari 2024

19:29:22
1434398

Guterres: Hali ya Gaza ni fedheha kwa ubinadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika hotuba yake siku ya Jumatano kwamba: "mauaji, njaa, kiu na uharibifu unaoshuhudiwa katika Ukanda wa Gaza ni fedheha kwa ubinadamu."

Antonio Guterres, kwa mara nyingine ameonya kuhusu hali mbaya ya Ukanda wa Gaza na kuongeza: "Lazima tuheshimu maazimio ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu na tuna wasiwasi kuhusu hali ya kibinadamu ya Wapalestina huko Gaza."

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) unapaswa kudumishwa na kusema: UNRWA ndio uti wa mgongo wa juhudi za kibinadamu huko Gaza.
Kwa upande mwingine, Martin Griffiths, Mratibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura amesema katika kikao cha Baraza la Usalama kilichofanyika jana kujadili hali ya Palestina kwamba: "Kila siku inayopita, inazidisha masaibu na mateso ya watu wa Gaza."Martin Griffiths ameeleza kuwa, mapigano makali yanayoendelea kandokando ya Khan Yunis yamewalazimisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao kuelekea Rafah na kusema: Eneo hili sasa linahifadhi zaidi ya nusu ya wakazi milioni 2.2 wa Gaza. Akiashiria kwamba zaidi ya 60% ya makazi ya watu yamebomolewa au kuharibiwa kote Gaza na kufafanua kuwa: Sasa tunakadiria kwamba karibu 75% ya jumla ya watu wa Gaza wamekuwa wakimbizi. Ripoti zinaonyesha kuwa, zaidi ya Wapalestina elfu 26 wameuuawa na maelfu ya wengine wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel.​

342/